PASAKA WA PILI NI
UREJESHO WA KUSUDI KUU LA KWANZA LA UFALME WA MUNGU.
SEHEMU YA 3
Damu
ya mwanakondoo ilipakwa kwenye miimo ya milango; na nyama (mwili) ya mwanakondoo
ililiwa na kila mwanafamilia (Kutoka
12:7-8). Nyama ya mwanakondoo ililiwa yote na hakuna hata kipande kilipaswa
kusazwa… Kumbuka damu na nyama (mwili) wa mwanakondoo ndiyo vilihusika katika
kufunika nyumba/wanafamilia! Damu na mwili!!!
Ishara kwenu
Ishara kwangu
Ishara kwenu: maana
yake ni kwamba, damu ilikuwa na kazi ya kuwapa uhakika/uthibitisho ya kwamba
mmo ndani ya uhusiano na Yehova, kwahiyo hamuhitaji kwenda mahala pengine
kutafuta uhusiano na usalama. Kwa damu hiyo ya Pasaka pekee mnapaswa kutulia
ndani kwani Yehova yuko kazini.
Maana
nyingine ni kwamba hii ni ishara ya kwamba ninyi nyote mzungukwao na damu ya
dhabihu ya Pasaka ni familia, ni kundi moja! Hebu jaribu kutengeneza picha
katika fikra zako (imagination) pale unapochungulia dirishani ama utokapo nje
na kisha kuona nyumba ya jirani nayo ina damu kwenye miimo yake kama ilivyo
yako… Naamini utasema “aah, kumbe naye ni mwenzangu”. Hivyo utaelewa kwamba
jirani yako amepata maelekezo sawa sawa na yale uliyoyapata wewe vilevile
utagundua ya kwamba jirani yako ni mtiifu kama ulivyo wewe- Haleluya!!!
Hivyo,
uhusiano anaouanzisha Mungu si wa siri… Anauweka wazi kupitia alama (ishara) ya
damu. Ishara (sign) si kitu halisi
bali huwakilisha kitu fulani kingine. Kwahiyo damu si kitu halisi cha mwisho
(not the end result), bali kuna jambo kubwa zaidi ya damu. Yaani kuna kitu
kingine kikubwa ambacho kinawakilishwa na ishara ya damu…. Damu ilikuwa na kazi
maalum ya kuwakilisha agano/makubaliano/mkataba ya kwamba “Ninawalinda katikati
ya uangamivu huu kwasababu ninataka uhusiano (fellowship) na ninyi.”! Umeelewa
kitu ulichokisoma? Ni hivi, damu siyo Hitimisho bali ni ishara na ishara
huwakilisha kitu kingine. Kwahiyo, hupaswi kuyaelekeza macho yako kwenye damu
tu bali kwenye ujumbe unaobebwa na damu… Kwahiyo, damu ya Pasaka ilikuwepo
kuwalinda waIsraeli ili wawe huru kutoka kwa wamisri kisha wapate nafasi ya
kuanzisha mahusiano/ushirika wa kudumu na Yehova! Mungu, Roho Mtakatifu, akusaidie
uone kwa namna hiyo!
Ishara kwangu Kutoka 12:13b,
“…nami nitakapoiona ile damu….”… Hii maana yake ni
kwamba damu ya kwenye miimo inazungumza kwa niaba ya waliomo ndani. Damu ni
mwakilishi/wakili wa wote inaowafunika! Hawakuhitaji kutoka nje ya nyumba zao
na kusema maneno mbele ya malaika wa kifo ili kumshawishi asifanye uangamivu
juu ya nyumba yao, bali damu ilizungumza na malaika kwa niaba yao! Kwa maneno
mengine, damu ilisema na Mungu kwa niaba ya watu… Hebu niruhusu nikutazamishe
maeneo (aspects) ya uwakilishi wa damu:
ü Kwasababu
wamisri wamekataa kutoa ruhusa ya uhusiano kati ya Mungu na taifa lake, nchi
nzima inapokea pigo… Sasa, kazi ya damu ni ni kunena na kuziambia mbingu ya
kwamba, “waliomo ndani ya nyumba hii tuna uhusiano nao…. Passover, Passover…”. Malaika wa kifo ikabidi apite bila kufanya
uangamivu !
ü Vilevile
damu ina kazi ya utambulisho na uwakilishi – ni kama vile damu
inawakilisha/inasema “hapa amechinjwa Pasaka…”
Kwahiyo
kupitia damu hii ya Pasaka Mungu aliwanunua waisraeli kutoka Misri si tu ili
awapeleke Kanani, nchi ya ahadi, bali ili ajenge uhusiano nao. Na ndiyo maana
hakuwapeleka Kanani moja kwa moja bali aliwapitisha jangwani miaka arobaini ili
kuujenga uhusiano. Ni muhimu sana hii dhana uikumbuke kwenye maisha yako yote
ya kwamba Mungu hakuwa anatafuta watu wa kuijaza au kuikalia nchi ya Kanaani
kwasababu walikuwapo wakaazi katika nchi hiyo. Wala hakuwa anatafuta kitu
kingine chochote isipokuwa
MAHUSIANO/USHIRIKA! Ndiyo kusema usuli (essence) wa sadaka ya Pasaka ni Mungu
kutaka kuwa na mahusiano kati yake na watu wake- JAMBO HILO HALIJABADILIKA HATA
SASA!
Ufalme wa Mungu ni nini?
Soma
kitabu cha Mwanzo sura ya 1 na ya 2
Utaona
Mungu alifanya uumbaji wa dunia na vitu vyote vilivyo ndani yake kwa utashi
wake mwenyewe, bila kushauriwa, kuombwa ama kulazimishwa na yeyote yule.
Aliumba kwa utashi na mapenzi yake mwenyewe na kwakusudi lake mwenyewe.
Baada
ya kufanya shughuli kubwa ya uumbaji wa dunia na kila kitu kilichomo ndani yake
kiijazacho dunia kwa muda wa siku tano kwa njia/malighafi (raw material) ya
neno la kinywa chake, siku ya sita anaamua kufanya uumbaji kwa kutumia mikono
yake. Baada ya kuumba kwa siku sita anaamua kutoa maelekezo kwa kiumbe chake
cha mwisho na maelekezo hayo ni kutawala…
Hakuna aliyemshauri, aliyemuomba wala kumlazimisha Mungu bali aligawa utawala
kwa wanadamu kwa utashi wake mwenyewe. Kutawala (rule) ni neno la kifalme na si
la kidemokrasia! Kwahiyo basi, Mungu anaamua kuyagawa baadhi ya madaraka yake
ya kutawala kile alichokiumba… anaamua kuyagawa kwa mwanadamu! Anaamua kugawa
kiasi cha madaraka yake juu ya uumbaji wake kwa mwanadamu. Mungu hakuwa
anaanzisha utawala wake bali alikuwa anafanya mwendelezo (extension) wa utawala
wake… Hii itakupa kusoma habari ya Mwanzo na uumbaji kwa jicho la tofauti
kabisa! Ninamaanisha, kila Ukisoma na kuona jinsi mambo yalivyoanza, nakushauri
usijisahau na kudhani kuwa na Mungu naye ndiyo alikuwa anaanza- HAPANA!
Alikuwepo kabla ya Mwanzo sura ya kwanza!
Mungu
aliuumba ulimwengu kwa mifumo miwili: ulimwengu
wa mwili na ulimwengu wa roho (Rejea kitabu changu Wokovu ni Uhakika wa Maisha ya
sasa na ya Baadaye ):
·
Ulimwengu wa mwili huongozwa kwa
mwili wakati ulimwengu wa roho huongozwa kwa roho
·
Ulimwengu wa mwili huwasiliana kwa
mwili wakati ulimwengu wa roho huwasiliana kwa roho.
·
Ulimwengu wa mwili una mwanzo na
mwisho (ni wa muda) wakati ulimwengu wa roho hauna mwanzo wala hautakuwa na
mwisho (ni wa milele)- Dhana ya muda, majira na nyakati hufanya kazi kwenye
ulimwengu wa mwili PEKEE!
·
Ulimwengu wa mwili huongozwa na
kutawaliwa na ulimwengu wa roho. Yaani ulimwengu wa roho ndiyo huamua nini
kitokee katika ulimwengu wa mwili.
Lengo
langu kukupitisha hapa ni ili kujibu baadhi ya maswali kadhaa, mojawapo ni lile
Mungu alikuwa wapi wakati akifanya shughuli ya uumbaji?
Mungu
alikuwa katika ulimwengu wa roho (usio na mwanzo wala mwisho, ambao huamua nini
kitokee katika ulimwengu wa mwili) wakati akiumba dunia na vitu vyote
viijazavyo (yaani ulimwengu wa mwili). Sasa pointi ya msingi nitamaniyo
ujifunze hapa ni ile yenye swali kuwa Kwanini Mungu aliamua kwa utashi wake
mwenyewe kumpa mwanadamu kuitawala dunia? Hii ni kwasababu mwanadamu ndiyo
kiumbe pekee chenye uwezo wa kuishi na kufanya kazi katika ulimwengu wa roho na
ulimwengu wa mwili kwa wakati mmoja (simultaneously). Kumbuka ufalme wa Mungu
una makao makuu katika ulimwengu wa roho na matawi/mwendelezo katika ulimwengu
wa mwili… Hii ni kwasababu mwanadamu ni roho yenye nafsi inayoishi ndani ya
mwili (Rejea Wokovu ni Uhakika wa Maisha ya Sasa ya Baadaye uk. 12-16). Kwa
ufupi kabisa hayo ndiyo maelezo ya jumla ya ufalme wa Mungu na nafasi ya
mwanadamu katika huo.
0 comments: