Monday, May 19, 2014

HAZINA YA MAARIFA NA FRED MSUNGU.

By Jimmy  |  12:35 PM No comments


(FUNZO KUU SIMAMIZI) KIINI CHA SOMO
 
(Hesabu 13:30-31)

 Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

  Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.

Ukisoma mstari wa 30 hapo utagindua kwamba pamoja na chanzo cha taarifa cha kwanza kua kibaya......! Kuna chanzo kingine cha taarifa ambacho kilijitokeza na walikua na nafasi ya kubadili chanzo kibaya na kuamini katika taarifa nzuri au kubadili maamuzi lakini hawakufanya hivyo.Hivi ndivyo inavyotokea hata katika maisha yetu ya kila siku, Kuna watu wamekufa na ndoto zao nzuri kwasababu tu walikataa au hawakutaka kukubali kulipa gharama ili kuyafikia mafanikio kutokana na kuamini taarifa mbovu walizo pokea. Mara zote kwenye maisha ya mtu mwenye malengo (dreamer)
changamoto hua zinatokea mara nyingi, Lakini pamoja na hayo yote hua kuna kua na chanzo kingine cha taarifa ambacho hutangaza kinyume na taarifa ya kwanza.Sasa hua kuna kua na gharama ya kulipa ili kuigeuza hali mbaya kua hali nzuri na hapa ndipo watu wengi wenye malengo au ndoto hushindwa kutimiza kutokana na kutokukubali kulipa gharama..hii inaweza ikawa ni kwenye biashara, kazi, shule, huduma na sehemu nyingine nyingi.Watu wengi wamekufa na ndoto zao ilipofika mahali wanatakiwa kufanya maamuzi ya kulipa gharama, Na hii hua ndio ile sehemu ya ushindi inayomfanya mtu kua mkuu, ni baada ya kutoboza upande wa pili.Na hii kamwe haiwezi kutokea kama hujaamua kubadili chanzo cha taarifa ambacho kitakusaidia kuibadili hali mbaya kua nzuri, kushindwa kua ushindi au hasara kua faida.

Jambo la kubadili chanzo cha taarifa ili uweze kubadili matokeo hua si swala la uwingi wa watu au ni watu wangapi wanasema nini, Hili hua ni swala na mtu binafsi na kile anachokiaona ndani yake kama vile jinsi Joshua na Kalebu pamoja na umati wote ule jinsi walivyoiamini taarifa ile lakini wao waliamua kua kinyume na kubadili chanzo cha taarifa na matokeo yao yalibadilika pia,Wakati umati wote ule wa watu waliipoteza nafasi ya kuiona Kaanani ila wao wawili walipata nafasi na ndio walioingia na kuimiliki nchi ile.Hivi ndivyo inatokea hata kwa maisha yetu ya kila siku ni wengi ambao walianza biashara,shule,kazi au huduma kwa pamoja wakiwa na wazo moja la kufanikiwa lakini ni watu wacahache sana ndio hufikia kile kilele cha mafanikio na kaona zile ndoto zao zimetia na kua kweli(.BADILI CHANZO CHA TAARIFA...Jinsi ulivyo leo ni matokeo ya kile ulichosika na kuamini)

Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0653-318117, ama kwa barua pepe fredymsungu@gmail.com 



Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP