Monday, May 5, 2014

HAZINA YA MAARIFA NA FRED MSUNGU.

By Jimmy  |  7:04 AM No comments

 SAFU YA FRED MSUNGU: BADILI CHANZO CHA TAARIFA
JINSI ULIVYO LEO NI MATOKEO YA ULICHOKISIKIA NA KUKIAMINI
SEHEMU YA TANO.....

      I.            NINI CHANZO SAHIHI CHA TAARIFA?
Unapokua na mawazo makubwa juu yako chanzo sahihi cha taarifa kwako ni wale watu ambao walikua na ndoto kama wewe na wamefikia malengo (wamefanikiwa) Kwasababu si wote waliokua na ndoto kubwa waliweza kuzitimiza...!halijalishi ni sababu gani iliowapelekea wao kushindwa,Inawezekana kua ni sababu  ya  msingi au si ya msingi lakini kama malengo hayakutimia jibu ni rahisi kwamba ameshindwa.Sasa watu wa namna hii wakati mwingine hua si watu sahihi sana kwako kwasababu kuna wakati hutumia vile vigezo vilivyowafanya wao kushindwa kwa kudhani kua haiwezekani kwa mtu mwingine kupenya na kufanikiwa. Lakini si kweli...! Kama wewe kuna mahali ulishindwa au ulianguka haimaanishi kila mtu hataweza kufika mahali hapo, Inawezekana wewe ulishindwa lakini yupo atakaeweza .Na hichi kitu ndicho kinatusababishia utofauti katika maisha, Tija si kua na ndoto nzuri kama ndoto nzuri kila mtu anazo..Muhimu hapa ni nani yuko tayari kupigana mpaka kuona malengo yake yakitimia na kua katika ulimwengu halisia na huu ndio ushindi ambao unamfanya mtu kua mkuu. (Mwenye mafanikio)

NINI CHA KUFANYA UNAPOHISI KUSHINDWA KUTIMIZA LENGO

Swala la kushindwa kufanya jambo si swala la ajabu na wala si geni...Hata watu tunaowaona wanamafanikio leo si wote ambao walianza safari ya kuzitimiza ndoto zao wakafanikiwa moja kwa moja hapana! Kukosea, kuanguka kupo lakini kikubwa ni nani yuko tayari kukomaa mpaka kuona matokeo ya kitu kinafanyika, na huyo sasa ndio hua mshindi. Makosa ni sehemu ya binadamu lakini wapo walioshindwa wakakata tama kabisa, Lakini pia wapo waliokutana na changa moto zikawarudisha nyuma lakini hawakukata tamaa, Kukata taaa ni sifa ya mvivu.Usijipe udhuru kwa sababu ya mazingira ulionayo au makosa uliyowahi kuyafanya yakakurudisha nyuma bado nafasi ipo ya kufanya makuu...Ukianguka tafuta chanzo cha taarifa kitakachokueleza namna ya kuinuka na kuendelea na safari.

.....................................................................................



(NI KHERI KUA NA NDOTO MOJA ILIYOTIMIA KULIKO KUA NA NDOTO ELFU ZISIZO NA TIJA)

MUHIMU: Ni vizuri kujifunza kutoka kwa watu ambao unahisi unafanana nao au wale watu wa aina yako. Ninaposema kujifunza sina maana ya kuiga la hasha..!Maana yangu hapa ni kuangalia ni njia zipi walizopita wao wakafanikiwa, Na je ni changamoto zipi walikumbana nazo na jinsi walivyozivuka. Kwanini ni muhimu kujifunza toka kwa watu wa aina yako? Inawezekana ni kweli mtu anamafanikio na amefika mbali lakini si kila mtu ni sahihi kwako

Mfano: Wewe una ndoto ya kuja kua mfanyabiashara mkubwa lakini mtu unaemfuatilia sana ni mchezaji mpira na unampenda kweli unapenda maisha yake na jinsi alivyofanikiwa... Rafiki haijalishi unajuhudi gani au mapenzi gani na hyu mtu lengo lako la biashara utafeli tu kwasababu kama lengo lako ni biashara basi mwana michezo si mtu sahihi kwako hata kama kafanikiwa kwa kiwango kikubwa aina gani.Mtoto wa simba ukimuangalia kwa mbali kuna wakati kama anafanana na paka lakini kiuhalisia Yule ni samba,Hawezi kua paka hata siku moja .Nyati kamwe hawezi kua ng’ombe japo maumbile ni kama sawa lakini tabia za hawa viumbe ni tofauti sana Hivyo ndivyo ilivyo pia hata katika maisha tunayoyaishi watu sahihi kwako ni wale unaofanana nao japo watu wengi kwenye sekta mbali mbali wanamafanikio lakini mtu sahihi kwako si yeyote aliefanikiwa.JIAMBATANISHE NA WATU SAHIHI UPATE MATOKEO SAHIHI.

NJIA MBALI MBALI ZA KUJIFUNZA

·        Kusoma vitabu mbali mbali vilivyoandikwa na watu hao au makala zao.

·        Kusikiliza/kuhudhuria semina, maongezi hamasishi na mahojiano yao mbali mbali.

·        Kufuatilia aina ya maisha wanayoyaishi(Mtindo wa  maisha)

Vitu hivi vikiwa kama chanzo cha taarifa yako baada ya kujitambua wewe ni nani na unataka nini vitausaidia ubongo wako kuanza kubadili fikra na mfumo wako wa maisha utabadilika kwasababu kuna vitu ambavyo ni lazima utaanza kuviamini na kuvitendea kazi ,Na kama una uhakika na chanzo chako cha taarifa kua ni sahihi basi kwa hakika mafanikio ni fungu lako.Somo hili litaendea J/tatu ijayo,usikose kuendelea kufatilia safu hii iliyoandaliwa na Fred Msungu.Kwa mawasiliano zaidi piga simu No 0653-318117 au fredymsungu@gmail.com.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP