Aliyekua mchezaji wa simba kwa miaka mingi aliyepata umaarufu kwa timu
alizo wahi kuzichezea kama Pamba ya Mwanza na Simba (Ntenze John Lungu) blog ilipata taarifa za mchezaji huyu kuokoka.Blog ilimtafuta Shaffih Dauda mtangazaji wa Sports extra ya Clouds fm 88.5 dar ambaye ameijuza blog kuhusu mchezaji huyu aliyeamua kumpa Yesu maisha yake na kuamua kutembea katika njia impasayo Mungu.Ntenze ameokoka na sio Nteze yule niliyekua nikimjua kwa miaka yake ya uchezaji wa mpira alisema Shaffih Dauda...Kwa sasa Ntenze John Lungu anaishi Marekani akiwa anafanya kazi Microsoft.
Nteze alianza kuichezea timu ya Pamba FC mwaka 1990 na mwaka 1994 akasajiliwa Simba SC hadi alipokwenda Afrika Kusini na Marekani kuchezea soka la kulipwa.Nteze alirejea Simba SC mwaka 2002 na baada ya hapo alistafu na kwenda kuishi Marekani.Nteze ni kati ya wachezaji wachache waliopata mafanikio wakiwa klabu na timu za taifa pia.
Shaffih Dauda alipokutana na Nteze John Lungu Marekani...Asante Shaffih kwa info za nguvu kwenye www.unclejimmytemu.blogspot.com.One love
0 comments: