PASAKA WA PILI NI
UREJESHO WA KUSUDI KUU LA KWANZA LA UFALME WA MUNGU.
SEHEMU YA 2
Nguvu
na kwa msisitizo ni hili: Kilichomfanya Mungu aanze mpango wa kuwaokoa taifa
lake teule si wingi wa maumivu yao, si ukubwa wa kilio chao, si masikitiko yao
bali ni AGANO yaani
mkataba/makubaliano aliyoyaweka na malango ya taifa la Israeli yaani Ibrahimu,
Isaka na Yakobo (Israeli). Soma vizuri kwa umakini (Kutoka 2:23-25). Agano aliloliweka Mungu na taifa la Israeli
lilianzia kwa baba wa mataifa yote Ibrahimu (Soma Mwanzo 22:15-19)
Kinachomvuta
Mungu si kilio! Unaweza ukajiliza muda mwingi sana, halafu Mungu anakutazama tu
kwasababu wingi wa machozi si chochote… Wakati mwingine Mungu anaamua tu
kuchukuliana na sisi katika upumbavu na kutokujua kwetu, lakini kama “tai”
unapaswa kujua ya kwamba Mungu hufanya kazi kwa kanuni na moja ya kanuni ni hii
“Mungu hulitazama neno lake ili alitimilize”
Kwanini Mungu anataka Israeli watoke utumwani?
Kutoka
3:18
Ukisoma
kwa jicho la kujifunza utagundua kuwa sababu kuu ya kutoka utumwani kwa wana wa
Israeli ni kwenda kumtolea dhabihu
Mungu wetu. Hicho ni kiashiria ya kwamba kwa kipindi chote cha utumwa na ufalme
mwingine, wana wa Israeli hawakuwa wakimtolea Mungu dhabibu/sadaka.
Unaweza
kujiuliza dhabihu/sadaka ni nini? Ina umuhimu gani kiasi hiki mpaka Mungu aamue
kuanzisha harakati za uhuru wa taifa ili tu apate hicho kitu kinaitwa
dhabihu?... Dhabihu ni ibada inayoonyesha hali ya mahusiano kati ya mtoaji na
mpokeaji wa dhabihu. Pia ni njia aitumiayo mtoaji wa dhabihu kumtambua mpokeaji
wa dhabihu kuwa ni mkuu katika maisha yake.
·
Ni shughuli ya kiroho (katika
ulimwengu wa roho – si ulimwengu wa mwili)
·
Ni ibada ya kiushirika
(fellowship)- mahusiano binafsi; mahusiano ya karibu (communion)
Wana
wa Israeli walikosa kufanya tukio hili muhimu kwa kuwa walikuwa katika hali ya utumwa
na chini ya ufalme.
Hivyo
basi, Mungu anadai mahusiano na watu wake (taifa lake teule) na mahusiano hayo
yanatakiwa kujengwa na kustawishwa katika mazingira huru (nje ya utumwa na
ufalme wa Misri). Mungu angeweza kabisa kuomba dhabihu ilihali wana wa Israeli
wakiwa Misri lakini hayo si mazingira sahihi ya kuyalea mahusiano yake na watu
wake. Ni muhimu ukumbuke kuwa mazingira yaliyokuwako Misri yalikuwa ni:
·
Fikra za kitumwa (slavery
mindset/mentality)
·
Miungu ya Misri
·
Ufalme wa Misri
·
Mabwana – wamiliki wa watumwa
Katika
mazingira haya, hakuna uhusiano wa kudumu ungeweza kustawi.
Kutoka
12: 1-51
Baada
ya Farao (mfalme wa Misri) kukataa kuwaachilia huru taifa teule la Mungu. Mungu
anaandaa mpango usiozuilika wa ukombozi kwa njia ya sadaka/dhabihu iitwayo
Pasaka. Wazo la jina la dhabihu/sadaka hii twalipata Kutoka 12:11… Ni Mungu
mwenyewe ndiye aliyetoa maelekezo kwamba sadaka hiyo iitwe Pasaka, si fikra za
Musa wala kiongozi awaye yote.
·
Mzaliwa wa kwanza
·
Asiye na mawaa
·
Asiye na ulemavu yaani mkamilifu
·
Wa kiume
Pia
jambo jingine la msingi kutazama hapa ni kwamba, mwanakondoo huyo wa Pasaka
hakuchinjwa hovyo hovyo tu, bali alichinjwa kimkakati (strategically). Ukisoma Kutoka 12:3-4 utabaini ya kwamba
mwanakondoo alikuwa ni maalum kwaajili ya kuihifadhi nyumba fulani na kama watu
wa nyumba walikuwa ni wachache basi walishirikiana na jirani zao… Maana yake ni
kwamba mwanakondoo mmoja alikuwa ni kwaajili ya kufunika idadi ya watu kadhaa –
Hii ni maalum sana.
nguvu

Pasaka wa kwanza ni nani/nini?

Sifa ya dhabihu ya Pasaka (Kutoka 12:5):

0 comments: