Madhumuni ya uanzishwaji wa kituo hiki ni kulea watoto yatima waliopoteza wazazi wao na hivyo kupelekea watoto hawa kukosa Elimu, Malezi bora, malazi, matibabu, na hata upendo. Hivyo kuweza kuwaepusha watoto hawa na majanga mabaya ya kidunia, kama uvutaji madawa ya kulevya, uasherati, n.k MIOCA imekua mstari wa mbele kuwasaidia watoto hawa bila kujali dini, kabila, wala rangi.
Mpaka sasa kituo hiki kimefanikiwa kupata watoto wapatao 94, wa kiume ni 54 na wa kike ni 40, ambao ni wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi, sekondari, na chekechea. watoto wote hawa tunaishi nao hapahapa kituoni chini ya usimamamizi wa mama mlezi bi. halima.
Ndugu watanzania wenzetu tunapenda
kuwafahamisha juu ya changamoto zinazotukabili . kwa sasa kituo kinakabiliwa na deni la hospitali katika hospitali inayoitwa MICO RABININSIA MEMORIAL HOSPITALI Iliyopo Namanga Tegeta, deni hili limetokana na matibabu ambayo watoto wamekuwa wakipata tangu february 2012 mpaka february 2014, tunadaiwa kiasi cha tshs 7,797,900/= msimamizi wa hospitali anaomba kupatiwa pesa, ili watoto waweze kuendelea kupatiwa tiba, tuna wakati mgumu katika kutimiza hili kwani ni uvumilivu mkubwa ambao ametuonyesha katika kuwasaidia watoto hawa hivyo tunawaomba ndugu wote mtakaosoma habari hii muweze kutuunga mkono. tuna imani kubwa sana kuwa ombi letu litapokelewa na kupatiwa ufumbuzi, kwa ushirikiano mtakaotupatia mtakuwa mmeweza kuwaokoa watoto hawa katika tatizo hili, kwani afya ni kitu muhimu katika maisha ya binadamu. ikizingatiwa watoto hawa hawana baba wala mama kwa hiyo wewe na yule mtakua ndio msaada pekee katika kuwaokoa watoto hawa.
mwisho tunapenda kuwakaribisha sana katika kituo hiki, ili kwa pamoja muweze kuwasaidia watoto hawa. kama maneno ya mwenyezi mungu yanavyotufundisha kuwa "HUDUMA KWA MWANADAMU NI HUDUMA KWA MWENYEZI MUNGU." asanteni sana na karibuni MIOCA'S
kwa mawasiliano zaidi,
0715720022, 0759090290.
A/c no. ni 01j2080397900 Mioca'S, bank ya CRDB Tawi la mbezi beach.
0 comments: