Kama ulipata bahati kuangalia kipindi cha
Chomoza ya Clouds TV jumapili iliyopita nilifanya mahojiano na Mamu
ambaye ni mkurugenzi wa Umoja audio vision kiwanda cha kutengeneza CD za
muziki wa aina mbalimbali ukiwemo wa injili.
Kiwanda
hiki kilichopo barabara ya Nyerere karibu Shoprite kinasambaza karibia
kazi za wasanii wote wa muziki wa injili.Mamu ni mtanzania wa kwanza
aliyeanza kazi ya usambazaji mwaka 1988 kwa kuanza na usambazaji wa
kaseti audio pamoja na DVD.
Kati ya
mambo niliyotaka kujua kutoka kwake ni muimbaji gani anafanya vizuri
kwenye soko la mziki wa injili hivi sasa.Hili lilikua swali gumu kwake
kwani yuko na waimbaji wengi hivyo kutokana na swali langu Mamu hakutaka
kuniweka wazi kwa sababu za kibiashara.
Lakini
kwa maneno yake
alijaribu kugusia muimbaji (Bahati Bukuku) kwa sasa
anahisi anafanya vizuri sokoni akifatia Ambwene Mwasongwe na Rose
Muhando.
Sikuishia hapo nilipita mitaa
ya kariakoo na kuongea na baadhi ya wauzaji wa rejareja wao walisema
katika soko la gospel Bahati Bukuku anafanya vizuri na albamu yake ya
"Dunia Hina Huruma" anafuatia Ambwene Mwasongwe na Rose Muhando.
Nikiwa na Manager wa kiwanda cha Umoja audio vision.
Mdau wangu ziko picha kadhaa za kiwanda cha Umoja audio vision
Manager wa kiwanda akinionyesha aina ya mastar CD inavyokua mwanzo kabla ya kuingia kwenye mashine
0 comments: