Nakushukuru Mungu, Umenitoa Mbali
kwenye shimo la dhambi, Sasa nafurahia ndani ya nyumba yako Baba Baba, sina cha
kukulipa. Haya ni baadhi ya maneno yanayopatikana katika wimbo maarufu unaoitwa
Nakushukuru Mungu ulioimbwa na Kwaya ya Vijana Msasani ambayo sasa inajulikana
kama Kwaya ya Ukombozi.
Kwaya hii ya Ukombozi ni moja
kati ya kwaya ambazo zimejipatia umaarufu mkubwa katika ramani ya muziki wa
injili na kumtukuza Mungu ndani nan je ya mipaka ya Tanzania.
Kwaya hii pia iliwahi kusikika
miaka ya mwishoni mwa 90 waliposhirikiana na muimbaji mkongwe Cosmas Chidumule
katika album ya Kiatu cha Yesu ambapo kwaya hii ilishiriki kuitikia nyimbo zote
pamoja na kupiga muziki katika album hii iliyotoa nyimbo maarufu kama Yesu ni
Bwana na Libarikiwe Neno.
Ukombozi
ilianzishwa rasmi mwaka
1977 na ina makazi yake katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
Usharika wa Msasani ikiwa na takribani waimbaji 50 ambao kwa pamoja wamenia
kumtumikia Mungu kwa kutumia vipaji vyao vya muziki na uimbaji.
Mwaka jana mwanzoni kwaya ya
Ukombozi iliingiza sokoni tena album ya video nyingine iitwayo Sabuni ya Roho
ambapo ndani yake kulikuwa na wimbo maarufu uitwao Ni Kwa Neema na nyinginezo
nyingi. Uzinduzi wa album hii ulishuhudiwa na wageni mbalimbali akiwemo Waziri
Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa aliyekuwa mgeni rasmi.
Mpaka sasa album ya Sabuni ya
Roho imeshauza nakala takribani elfu tano na inazidi kufanya vizuri chini ya
usambazaji wa kampuni ya Umoja Audio and Visual Company.
Kufuatia mafanikio haya kwaya hii
inayofundishwa na walimu watatu imeamua kufanya ibada ya pekee ya kumshukuru
Mungu siku ya tarehe 6 mwezi Aprili katika usharika wao wa nyumabani Msasani
ambapo wageni mbalimbali wamealikwa kuhudhuria ibada hii.
Uzinduzi wa Nakushukuru Mungu Utakavyo kua.
Sadaka ya shukrani itakwenda
sambamba na uzinduzi wa remix album ya Nakushukuru Mungu audio ambapo ndani
yake kuna nyimbo kama Usinipite, Sema Kitu na Nakushukuru Mungu ambao
umejizolea umaarufu miongoni mwa watanzania wengi.
Kwa mujibu wa mwenyekiti Bwana Mchome,
Ukombozi walifikia maamuzi ya kuurudia wimbo huu ili uendane na teknolojia ya
sasa maana watu wengi bado wanauhitaji na hivyo kwaya iliona ni vema kuitikia
wito.
Kama ilivyo kwa album ya Sabuni
ya Roho, Nakushukuru Mungu pia imefanyiwa kazi katika studio za CVC Chang’ombe
chini ya mtayarishaji Steven Deffa ambaye ametengeneza album nyingi
zinazofanya vizuri kama Usiku wa Manane
na Mtu wa Nne ya Kinondoni Revival Choir.
Hii ni siku ya muhimu kwao
maana Biblia inasema tumshukuru Mungu kwa kila jambo, hata kwa magumu
tuliyopitia bado kumshukuru Mungu ni jambo muhimu sana
Siku hii pia itajumuisha mualiko
wa waimbaji mbalimbali wa zamani waliombia kwaya hii ambapo wapo maaskofu kama
Stephen Munga wa Dayosisi ya Lushoto na Profesa Godwill Mrema wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam ambao hawa wote waliwahi kuwa wenyeviti huko zamani.
Kwa mwaka huu kwaya imedhamiria
kupanua mipaka ya kufanya huduma kwa kutembelea mikoa mbalimbali kumtangaza
Kristo na pia iko katika mchakato wa kupata basi la kutumuia kwa ajili ya
huduma yao.
0 comments: