Maendeleo Bank ni benki iliyoanzishwa na KKKT Dayosisi ya mashariki na pwani,ilianza kazi rasmi tarehe 6/9/2013 mwaka huu lakini mchakato wa kuianzisha ulianza Nov 2011.Ni
benki inayoendeshwa kwa kufuata taratibu zote za benki kuu...Inatoa
huduma
mbalimbali zikiwemo mikopo,akaunti mbalimbali zikiwemo akaunti za
watoto,vikundi vya wajasiriamali na watu binafsi.
Ni benki ambayo inahudumia
wananchi wote ikiwa na lengo kuu la kuinua vipato vyao kwa kutoa huduma
bora na nafuu,kuinua viwango vyao vya uchumi hasa wale wa kipato cha chini.Imezinduliwa rasmi leo na makamo wa Rais Dr Mohamedi Bilal.
Bank hii inatoa huduma nyingine
kama western union,pamoja na kutuma fedha ndani na nje ya nchi.Inatoa
mikopo kwa riba nafuu na mteja anafungua akaunti kwa gharama nafuu sana
kuanzia 5000.Wapo Luther house Azania front mtaa wa sokoine drive postar
mjini.
Dr Mohamedi Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi.
Wachungaji na Ma-Askofu mbalimbali walikuwepo
0 comments: