Friday, November 1, 2013

CHUKUA TIME YAKO KUSOMA KILICHO ANDIKWA NA GAZETI LA JAMBO LEO KUHUSU TB JOSHUA.

By Jimmy  |  12:38 PM No comments

 TB Joshua aliwahi kutabiri kifo cha Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na kuibua mjadala mzito kwa nchi za Afrika na kifo cha Rais wa Nigeria, Umaru Yar’Adua na tukio la ugaidi nchini Marekani ambalo lilitokea mwaka 2001.
 ‘TB Joshua’, ametabiri kuwa, Rais mmoja wa nchi za Afrika Mashariki atatekwa na shambulizi la kigaidi kutokea katika nchi hizo.   Nchi za Afrika Mashariki kwa sasa zinaundwa na Uganda inayoongozwa na Rais Yoweri Museveni, Kenya inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, Rwanda na Rais Paul Kagame, Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza na Tanzania Rais Jakaya Kikwete. Utabiri huo umekuja siku chache baada ya TB Joshua kutabiri kifo cha Rais mmoja wa nchi za kusini mwa Afrika, ambapo haikuchukua muda kikatokea kifo cha Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika.
Pia, TB Joshua aliwahi kutabiri kifo cha Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na kuibua mjadala mzito kwa nchi za Afrika na kifo cha Rais wa Nigeria, Umaru Yar’Adua na tukio la ugaidi nchini Marekani ambalo lilitokea mwaka 2001.
Mchungaji huyo wa Synagogue Church of All Nations (Scoan), alitoa utabiri wa rais mmoja wa Afrika Mashariki kutekwa mwezi uliopita mjini Nigeria, wakati akitoa mahubiri yake na kuacha taharuki kubwa kwa wananchi wa nchi hizo kuhusu ni rais gani atatekwa na shambulizi hilo litafanyika nchi ipi.
Akizungumza kwenye ibada hiyo kanisani kwake, Joshua alisema nchi ambayo ipo kwenye hatari ya kukutwa na tukio hilo ni ile iliyowahi kupatwa na matatizo wakati watu wake wakiwa wanakunywa na kucheza, huku akiongeza kwamba tukio hilo litatokea tena.
Ingawa hakutaka kutaja jina la kiongozi huyo wala nchi anayotokea, alisema ameambiwa na Mungu kwamba, endapo atamtaka kutaja jina la kiongozi na nchi atokayo, atafanya hivyo. Kutokana na hali hiyo, amewataka wananchi wa Afrika Mashariki kumuomba Mungu ili jambo hilo lisitokee.
Akitoa maoni kuhusu utabiri huo bila kutaja jina lake alisema: “imani ni hiyari. Yesu alituambia tutawajua kwa matunda yao, hivyo kama hufuatilii mahubiri ya TB Joshua na jinsi unabii wake unavyotimia, huwezi kuamini, lakini kama unafuatilia na bado huamini, basi muda wako kuamini haujatimia.
“Kama mnaamini unabii ulikuwepo, upo na utakuwepo hadi mwisho wa dunia, je, kwa nyie mnaobisha ni nabii gani mnayeamini ni mtumishi kweli wa Mungu?
“Manabii wapo na Mungu anaendelea kuleta miujiza kupitia wao ili tuamini kuwa,  yeye ndiye alfa na omega. Kama unasubiri nabii mpya azaliwe halafu wewe ndiyo useme huyu ndiyo nabii, basi subiri huo muujiza,” alisema.
TB Joshua ambaye ana wafuasi lukuki, aliwahi kutabiri kifo cha mfalme wa Pop duniani, Michael Jackson na kuangushwa kwa dikteta wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo na kweli ikawa hivyo.
Alipoulizwa wakati mmoja ni kwa nini hupenda kutabiri mambo mabaya, alijitetea kwamba, anafanya hivyo ili kuwatahadharisha wanadamu kujiweka tayari kwa kufanya matendo mema.
TB Joshua aliwahi kutoa mchango wa sh.milioni 25 zikiwa ni rambirambi kwa watu wa Zanzibar waliopata ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea miaka michache iliyopita katika bahari ya Hindi na kupoteza maisha ya zaidi ya watu 240.   Nabii Joshua  amekuwa na msaada mkubwa Nigeria, kwa watu wa mataifa mbalimbali kiroho na kimwili, ikiwa ni pamoja kutoa misaada kwa jamii. Husaidia wajane, yatima, walemavu na maskini na humrudishia Mungu utukufu kwa kila jambo linalotokea kanisani kwake.
Katika kanisa lake watu wanaokwenda kupata ibada, hupata maji ya upako ambayo watu huyachukua na kuyatumia katika maombezi yao na wengi wameshuhudia kufunguliwa katika matatizo yao.   Muft Simba
Wakati huo huo, Magendela Hamisi anaripoti kuwa, Muft wa Tanzania, Sheikh Issa Shaban bin Simba ameishauri Serikali kuwalinda wananchi wake sanjari na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini kujilinda na changamoto hiyo.
Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana baada ya kujibu swali lililomtaka kuweka wazi namna Waislamu wakatakavyoweza kujilinda katika mikusanyiko yao katika shughuli za ibada na nyinginezo kutokana na tishio la kigaidi lililopo katika nchi za Afrika Mashariki.
“Katika suala la kujilinda kutokana na tishio la kigaidi tunaichia Serikali, nikiamini kuwa ina wajibu mkubwa wa kufanya hivyo, lakini pia tunahitaji kuisaidia kwa kutoa taarifa zinazoashiria hayo.
“Hatujilindi kwa vita wala kujibu kutokana na matukio ya kigaidi na hatutaacha kufanya ibada kutokana na kuwepo kwa hali hiyo, tunaomba Serikali ijitahidi kuweka ulinzi kwa kuwalinda watu wake, nasi tunahitaji kuisaidia ili kulinda amani ya nchi yetu,” alisema.
Mufti Simba aliweka wazi kuwa katika shughuli hiyo ya kutimiza ibada ya Hijja, Mtanzania mmoja kutoka Mkoa wa Singida alipata matatizo ya afya baada ya kupata tatizo la ubongo lakini alihudumiwa vema na madaktari.   Alifafanua kuwa afya ya muumini huyo inaendelea vema na tayari amerejeshwa nchini kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) hadi hali yake itakapotengemaa.
Simba aliongeza kuwa licha ya dosari hiyo kujitokeza Hijja ya mwaka huu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuwa sehemu ya kujivunia na kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha safari hiyo muhimu.   Pia Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema ni vizuri Waislamu wote nchini wakaendelea kudumisha amani na utulivu na kuishi kwa upendo na jamii mbalimbali bila kujali tofauti za dini.
“Waislamu wote waliokuwepo Makkah waliishi kwa upendo na watu wa mataifa mbalimbali duniani hali ambayo inapaswa kuendelezwa nchini ili kudumisha amani na utulivu uliopo kwa maslahi ya taifa,” alisema.
Source: Jambo leo

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP