Mtume Jeremia Mwakanyilenge akiwa ofisini kwake.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake
Kwakua Mitume wa kweli wao ni wahudumu wa jamii na Mungu hufanya mambo magumu kuwa mepesi.Hayo yamesemwa na mtume Jeremia Mwakanyilenge wa huduma ya 'Jem ministry' ya jijini mbeya aliopokuwa akiitambulisha huduma hiyo kwa Bloger na waandishi wa habari ofisini kwake.
Mwakanyilenge amewataka waumini kuwa makini sana na huduma hizi zilizoshamiri zinazo ibuka kila siku kutokana na kuwepo na baadhi ya watumishi matapeli wanaotumia jina la kristo kujinufaisha wenyewe binafsi
"Ukiona mtume huduma yake inaleta uchochezi katika taifa hili ujue huyo si wa Mungu atakuwa amejituma mwenyewe na ni tapeli,kwani aliyetumwa na Mungu kweli huyafanya yaliyo magumu kwa watu kuwa mepesi alisema mwakanyilenge.Katika kaikao hicho na waandishi wa habari pia alipata nafasi kutambulisha huduma yake ya Jem Ministry kua si kanisa jipya bali ni taasisi ya kuihudumia jamii kwa kuwapatia ajira watu katika idara zake za biashara kama vile JP PRODUCTION STUDIO inayofanya kazi za kurekodi audio cd pamoja na video,lakini imeanzisha mfuko wa kustaafu wachungaji.
0 comments: