Friday, March 15, 2013

KWA TAARIFA YAKO HAYA NDIYO ASIYOYAPENDA PAPA MPYA WA KATOLIKI.

By Jimmy  |  11:29 AM No comments

Kushoto ni  Pope Benedict XVI aliye mpatia kijiti Papa mpya 2013 "Francis wa kwanza"
Baba Mtakatifu mpya, Francis wa Kwanza, anatofuatina na viongozi 
 wengine wa Kanisa Katoliki kwa mambo mengi. Kama Askofu Mkuu wa Buenes Aires hakutaka kuishi kwenye kasri na wala hakutaka kuwa na dereva. Aliishi katika makaazi ya kawaida na alipanda basi kama watu wa kawaida.
Baba Mtakatifu huyo mpya mwenye umri wa miaka 76 alipenda kujipikia chakula chake mwenyewe. Sifa yake kama kiongozi mwenye unyenyekevu ilithibitika juzi katika kauli zake za kwanza.
Alitokeza akiwa amevalia vazi jeupe la kipapa na mbele ya maelfu ya waumini waliokuwa wanashangilia kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro, makao makuu ya Vatican, lakini badala ya kuwabariki watu kama ilivyo desturi, ni yeye Papa Francis aliyewaomba waumini wamsalie.
Waumini wa Kikatoliki wakishangiria mjini Buenos Aires, Argentina, baada ya Francis I kutangazwa kuwa Papa. Waumini wa Kikatoliki wakishangiria mjini Buenos Aires, Argentina, baada ya Francis I kutangazwa kuwa Papa.
Wazazi wa Papa Francis wenye nasaba ya Kitaliano, walihamia Argentina miaka kadhaa nyuma. Kiongozi huyo mpya wa Kanisa Katoliki anasemekana kuwa ni shabiki wa kandanda, muziki na ana sifa kubwa ya kuwa mtetezi wa masikini, na hivyo anatarajiwa kuzigusa nyoyo za watu kwa unyenyekevu wake.
Lakini pia, kama walivyo mapapa wengine waliotangulia, naye pia ni mhafidhina. Katika miaka ya nyuma aliwahi kukwaruzana na Rais Christina Kirchner wa Argentina juu ya masuala ya mashoga, pale mwaka 2010 alipoziita ndoa za jinsia moja kuwa ni njama za kuuteketeza mpango wa Mungu.
Pia Papa Francis wa Kwanza anapinga utoaji mimba na wanawake kuwa makasisi. Lakini pia inapobidi anatofuataina na viongozi wenzake wa kidini. Amewahi kuwalaumu waziwazi baadhi ya viongozi hao kwa unafiki na waliosahanu kwamba Bwana Yesu aliwatibu wakoma na alikula chakula pamoja na makahaba. Francis wa Kwanza ni Baba Mtakatifu wa 266 anayechukua nafasi ya Papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwezi uliopita
Hizi ni picha za baadhi ya watu wakifurahi baada ya kumuona Papa Francis

 


 Wengine hawaamini!!
Baada ya Papa Francis kutangazwa na hatimaye kujitokeza kwenye maelfu ya watu,Mama huyu alishindwa kuvumilia akaangusha chozi.



Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP