Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka Bwana Alex Msama amevieleza vyombo vya habari siku ya jana mpaka sasa waimbaji wa wili Rose Muhando na John Lisu wamepata kura nyingi katika kutumbuiza siku ya Pasaka,hivyo tayari kamati yake imewapitisha kushiriki tamasha hilo.
Rose Muhando na John Lisu.
Kwa sasa bado tunaendelea na mchakato wa kura ya maoni kwa mashabiki wetu kwa njia ya kutumia ujumbe mfupi wa maandishi au kupiga simu kueleza ni waimbaji gani wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania wanaotaka wawepo kwenye tamasha la mwaka huu.
Dhamira ya tamsha letu mwaka huu ni liwe la aina yake na tuwashirikishe mashabiki wetu,ndiyo sababu kuanzia mikoa litakapofanyika mpaka suala la waimbaji tumewapa fursa mashabiki wenyewe wateue;alisema Msama na kuongeza kuwa msanii atakayekuwa amepigiwa kura kwa wingi ndiye watakayemtangaza.
0 comments: