Paul Clement
Ni kijana Mpole ambaye ukikutana naye kwa mara ya kwanza huwezi juwa nini Mungu ameweka ndani yake PAUL CLEMENT Kijana wa Chang'ombe Maduka mawili Dar es salaam.Leo kupitia face to face ya Intarview na Uncle Jimmy ameweza kueleza mafanikio ya kwake ya muziki wa injili na wapi kwa sasa kimuziki.
Kwa sasa Paul yupo Kundi la GLORIOUS CELEBRATION lakini kupitia hatua nyingine amekuja na ujio wa Albam yake mpya inayokwenda kwa jina (NO JESUS NO LIFE) Album hii amefanya shukrani kwa Mungu kutokana na vitu ambavyo alikuwa akipitia hapo nyuma.
Wakati akifanya nyimbo ya juu ya "Mataifa yote" amabayo iko katika albamu ya Glorious Celebration alikuwa amefukuzwa nyumbani na Baba mzazi hivyo alihangaika sana ndipo alipo pata ufunuo wakuandika Record ya Juu ya Mataifa,Kuanzia hapo maisha yalikuwa magumu sana,aliishi kwa shida.
Katika hali ngumu aliyokua akipitia kijana Paul Mungu alimuinulia Mtumishi wakumsaidia ambaye mpaka sasa bado yuko kwake Askofu Mwakanga'ta.
Jembe linalotisha on the stage.
Kwa sasa Kijana Paul kipenzi cha Wadada yuko na Album yake ambayo ina nyimbo 8 na katika nyimbo hizo amemshukuru Mungu na kuzungumzia ukaribu wake na Mungu,pia ameandika nyimbo hizo katika hali aliyopitia wakati huo.Kurecord kwa nyimbo zake ilimchukua miaka mitatu mpaka kukamilisha album japo alipata shida katika kupata pesa yakufanyikisha album hii.
Yupo mtu ambaye awezi msahau katika maisha yake ambaye alichukua muda wake kumfundisha kuimba ambaye ni Mwanamuzi wa mziki wa Bongo Fleva (Ben Pol) yeye amekuwa mchango mkubwa kwa Paul katika kumuelekeza jinsi ya kuimba na kufanya Sauti kuanzuri.
Paul Clement anaendelea kusema kama muimbaji (Ben Pol) asingehusika katika kumfundisha muziki basi leo angekuwa mvuta bangi au mtu wa kula madawa ya kulevya,lakini kwa Mungu kuna kila kitu kikubwa ni uzima na kumsikiliza yeye nini anakupa ufanye kwa majira yake.
Album hii ya "NO JESUS NO LIFE" amefanya Studio ya MAWILASON STUDIO iliyoko Chang'ombe,soon Album atakuwa akisambaza mwenyewe.Ka tayari kupata album hii
0 comments: