Jiji la Mwanza lina uzuri mkubwa wenye vivutio vingi kwenye kila kona.Wenyeji wangu siku ya leo hawakuacha kunizungusha kila kona kujionea baadhi ya vivutio vya utali pamoja na maonyesho ya Este Africa yanayo endelea hapa mkoani Mwanza.
PICHA 7 YA MAONYESHO YA EST-AFRICA YANAYO ENDELEA VIWANJA VYA NYAMAGANA
Moja kati ya kivutio kikubwa kwa sasa Mwanza ni kivutio cha Maonesho ya wanyamapori walio hai kwenye Zoo iliyopo eneo la Clinick.Sehemu hii imekuwa kivutio kikubwa kwa Watoto na hata watu wazima.
Twende sawa na matukio ya Picha
Hii ni sehemu ya kuegesha magari,usihofu ukiwa na usafiri wako
Hapa Simba alikuwa akichokozwa kwa fimbo ili amke tumuone ukubwa wake.Usifanye mchezo na huyu mnyama,alitoa mngurumo mkali kila mtu alisogea hatua kumi.
Akiendelea kuchokozwa
Kwa mujibu wa mfugaji wa Simba huyu kwa siku moja anakula kilo za nyama 35 pamoja na lita za maji 25.Kwa sasa anamiaka 4.
Kiboko ya Swala Chui.Ni mnyama anae patikana kwenye Zoo ya hapa Mwanza.
PICHA 4 ZA JIJI LA MWANZA LINAVYO ONEKANA KWA SASA TOFAUTI NA MIAKA 20 ILIYO PITA
0 comments: