Askofu Malale wa Jimbo la Mwanza kitongoji cha Mji mwema mkudi wameanda mkutano wa injili ulio waalika wachungaji mbalimbali kutoka makanisa ya E.A.G.T ya mkoani mwanza.Mkutano huu ulioanza toka J/tatu ya wiki hii umekuwa wa baraka tele kwa wakazi wa kitongoji cha Mkudi.
Mwenyeji wa mkutano huu Askofu Malale alimualika Ev.Ernest Rwehabura toka Dar-es-salaam kuwa muhubiri wa mkutano huu mkubwa.Ukiacha wahubiri mbalimbali walio jitokeza katika mkutano huu pia waimbaji mbalimbali kutoka katika mikoa tofauti walikuwepo.Martha Mwaipaja-toka Dar
Tupone Kilembe-toka Arusha
Waimbaji wenyeji,Upendo Mkudi,E.A.G.T Mkolani Mwanza,na Magret Moses.Mkutano huu unatarajiwa kumalizika siku ya J/pili ya Tarehe 9/9/2012 majira ya jioni.Twende sawa na matukio ya Picha.
Martha Mwaipaja akiwa na Adolph Nzwalla asubuhi ya leo.
Huu ndio usafiri unao mpeleka na kumrudisha muimbaji Martha Mwaipaja kwenye mkutano huu unao endelea Mwanza.
PICHA 5 HIKI NI KIKUNDI CHA UWAMASISHAJI SHAMRA SHAMRA ZA MKUTANO.
Kazi kubwa ya kikundi hiki wakati mkutano unaanza waho upita kila kona ya karibu na mkutano wakiwa wanapiga filimbi huku wakipita kwa mbwembwe za madoido.
Twende kazi kushoto kulia filimbi mdomoni priiiiiiiiiii!!
Hii picha ukiiyangalia utadhani kama ndio wanaingia lahasha.Hapa wametoka kugeuza wanaendelea na zoezi zima la mnogesho wa Mkutano.
Hii timu ya vijana niliependa sana
Mchungaji mwalikwa mwenye suti nyeupe Rwehabura akipokelewa na mwenyeji wake Askofu Malale mwenye suti nyeusi kulia.
Mama Mchungaji Martha Mwaipaja akimtukuza bwana siku ya leo.
Katikati ni Mchungaji Daniel Moses kulola moja kati ya wachungaji wageni wa mkutano huu
Kulia Mtangazaji wa Alive Fm 91.9 Mwanza Adolph Nzwalla akikusanya habari za mkutano
Mchungaji Daniel Kulola akinionyesha Chapaa za sada ya mkutano.
Neno la kinabii likitamkwa
Kazi ya kuombea ikichukua nafasi yake kwa watumishi mbalimbali.
0 comments: