Ongoza kimkakati
Malengo ni nini?
Binafsi
nimekuwa na changamoto kubwa sana kutafuta maana rahisi na ya kueleweka juu ya
neno “malengo.” Huwa ninawaambia watu wengi ya kwamba inawezekana kwamba usiwe
na maana (definition) ya malengo, lakini ukiyaona ni lazima utayafahamu.
Lakini, huwa ninaamini ya kwamba huwezi kuanza kutenda/kushughulika na kitu,
jambo au hali usiyoijua. Na kwa misingi hiyo basi, ninawiwa kujenga ufahamu
ndani yako juu ya malengo. Katika mzunguko niliouonyesha hapa awali kwenye
taswira, malengo huzaliwa kutoka kwenye dhamira (utume). Lazima dhamira
ikusukume kuumba malengo! Sasa, malengo ni nini basi? Malengo ni ajenda au mahitaji husika/mahususi ambayo
mtu fulani hujiwekea kwa kipindi cha muda
fulani ili kumzalishia matokeo
yanayoonekana, matunda na/au mabadiliko yaliyokusudiwa… hupimika, huweza
kufanyiwa tathmini!
Weka malengo kwa vigezo hivi:
Malengo
mazuri huwa na sifa ya “SMART”, neno la kiingereza linalomaanisha nadhifu,
-enye uelewa mzuri. Kwahiyo malengo yako yanapaswa kuwa nadhifu, sasa neno smart
linabeba maana kubwa sana kwa kila herufi yake:
S -(Specific), kwanza lazima
lengo liwe ni maalum au hususani juu ya jambo, mtu au hali fulani. Kwa
mfano mtu anaposema, “Mimi ninataka kupambana na umaskini.”. Ni sawa hilo ni
lengo lakini si hususani, yaani halina mwelekeo… Je, mtu huyo anataka kupambana
na umaskini wa aina gani (umaskini wa kifikra, kifedha…), Je, anapambana nao
katika ngazi ipi? (mtu binafsi, kijiji, familia, nchi…) lazima uainishe. Na
ndivyo ilivyo katika huduma, unaweza kusema nina wito wa kuhubiri injili, ni
sawa lakini ni katika ngazi gani? Ni wazi kwamba kuizungukia dunia yote ni
jambo ambalo si rahisi (nchi zote, mikoa yote, majimbo yote, wilaya zote, vijiji
vyote na kaya zote za dunia.) Si jambo rahisi, ukijaribu utaumia tu na matunda
hayatakaa.
Mfano: Lengo langu ni kuihubiri injili nchini
Tanzania.
Kumbuka kuwa Tanzania ni nchi kubwa, ina mikoa zaidi ya ishirini na
wilaya zake na tarafa, kata, mitaa/vijiji na kaya (familia) kwahiyo unatakiwa
kuwa specific zaidi. Kwahiyo waweza kusema, kuhubiri injili nchini Tanzania
katika ngazi ya wilaya.
M -(Measurable), Pili lengo
lolote linatakiwa kupimika, Je unaweza kuuona ufanisi, matokeo au
matunda ya lengo hilo? Kwa mfano lengo la kuihubiri injili nchini Tanzania
katika ngazi ya wilaya…Baada ya muda je unaweza kupima matokeo ya lengo hilo. Sasa
kuna njia mbalimbali za kuyapima malengo yetu, baadhi ya njia ni kuangalia
mabadiliko katika maisha ya watu, je, kuna mabadiliko yoyote,njia nyingine ni
kuangalia je, idadi iliyokusudiwa imefikiwa? Tukiendelea kuutumia mfano wetu wa
kuihubiri injili nchini Tanzania katika ngazi ya wilaya ili tuufanye kuwa
SMART; Ili kuweza kupima lengo hilo waweza kusema:
Kuihubiri injili kwa watu 1000 nchini Tanzania katika
wilaya 4 (unapaswa kuzitaja wilaya ulizokusudia kuzifikia) kuanzia Januari
mpaka Juni.
0 comments: