Muimbaji mahiri wa muziki
wa Injili, Ephraim Sekeleti, atatumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya Kamata
Pindo la Yesu ya Rose Muhando Agosti 3, mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa
Rose Muhando jana, ilieleza kuwa tayari Kampuni
ya Msama Promotions
inayodhamini uzinduzi wake imeshamalizana na mwimbaji huyo.
“Nashukuru sana Msama Promotions kwa
udhamini wao, na jana (juzi) wamenihakikishia wameshamalizana na Sekeleti na
amekubali kuja kuungana nami katika uzinduzi wangu.
“Ni msanii mwenye uwezo mkubwa, ambaye
mashabiki wangu watapenda kuja kumuona jukwaani,” alisema mwimbaji huyo na
kuzitaja baadhi ya nyimbo maarufu za Sekeleti kuwa ni Uniongoze
na Kidonge cha Yesu.
Uzinduzi wa albamu hiyo utafanyika
ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Agosti 3, mwaka huu na kisha Agosti 10
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.Waimbaji wengine ambao hadi sasa
wameshathibitisha kushiriki uzinduzi huo ni Upendo Nkone, John Lissu na Bonny
Mwaitege, huku wasanii wengine mahiri wakitarajiwa nao kuthibitisha ushiriki
wao siku za usoni.
0 comments: