Akizungumza na gazeti hili katika
mahojiano maalum katikati ya wiki hii, Rose ambaye ameripotiwa kwa misala
tofauti ya kuchikichia fedha za shoo hivi karibuni, amefunguka kuwa afya yake
si nzuri kwani anasumbuliwa na mshipa kwenye mguu, akafanyiwa upasuaji katika
Hospitali ya Mkoa ya Dodoma.
“Siko vizuri kiafya
nimefanyiwa upasuaji mguuni, nimeshonywa nyuzi nne lakini bado hali yangu si
nzuri kiafya, nawaomba Watanzania waniombee,” alisema Rose kwa tabu na
kuongeza:
“Hata ukiniona
utanihurumia kwani mbali na upasuaji kwenye kidole gumba pia nimevimba sana
uso.
“Kwa sasa nipo kitandani nyumbani kwangu najiuguza. Nitarudi tena hospitalini Jumanne ijayo.”
Akizidi kumwaga maneno kwa kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, Rose alimshukuru mwandishi wa Barua Nzito iliyochapishwa katika gazeti tumbo moja na hili la Risasi Mchanganyiko (toleo lililopita) kwa kumuonya juu ya suala la kudaiwa kuingia mitini na fedha tofauti za shoo na kuomba radhi kwa Watanzania.

“Nawaomba sana radhi
wote niliowakosea, niwaombe waniombee nipone na nitarejesha fedha zao,” alisema
Rose.
Tunamuombea Rose kwa
Mwenyezi Mungu ampe afya njema ili aendelee na huduma ya kumtumikia Mungu kwa
njia ya nyimbo za Injili-Mhariri.
Chazo:BaabKubwa
BaabKubwa
BaabKubwa
0 comments: