Taarifa ya chanzo cha ajali ya Bahati Bukuku.
Mama wa maadili Bahati Bukuku (40) amepata ajali akiwa
kwenye gari alilokuwa akisafiria….Jeshi la polisi
linasema chazo cha ajali hiyo
gari ya Bahati Bukuku iliacha njia na kugonga gema baada ya kugongwa na gari lingine
linasomekana kuwa ni fuso.Watu wengine waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo mbali na
Bahati Bukuku ni watu wawili na gari lililopata ajali na kusababisha majeraha
kwa watu hao ni Toyota Nadia yenye namba za usajili IT 7945.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi David Misime amesema ajali hiyo imetokea July 25 saa tatu
alfajiri katika Barabara ya Morogoro-Dodoma eneo la Rach ya Narco wilayani
Kongwa.Uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea
0 comments: