Ongoza kimkakati
Kisa mkasa (Scenario) #2. Mchezo wa mpira wa miguu bila magoli.
Kama
wewe ni mpenzi, mshabiki au mfuatiliaji wa mchezo wa mpira wa miguu basi
uanelewa fika juu ya muundo wa viwanja vya mchezo huo… Moja ya vitu muhimu sana
kwenye ujenzi wa kiwanja ni milingoti minne mikubwa isimamayo pande mbili
tofauti (zinazokabiliana) za uwanja. Bila shaka umekwisha baini ya kwamba
ninazungumza kuhusu magoli.
Hebu
fikiri, mchezo wa mpira wa miguu pasipo magoli uwanjani… Je, inawezekana kuwa
na mchezo huo? Hata ule mpira wa “mchangani” huwa na magoli, hata kama ni ya
mawe au vijiti… Hauwezi kuwa mpira wa miguu bila magoli. Hebu jiulize wachezaji
wangekuwa wanakimbiakimbia uwanjani, wanapiga chenga, wanapeana pasi,
wanakaba/wanazuia mashambulizi… ili iweje sasa??? Kuna umuhimu gani wa kuwa na
mchezo wa mpira wa miguu pasipo magoli? Lengo kuu la mpira wa miguu ni magoli. Ukiyatoa malengo hayo, umeondoa
maana, umeondoa thamani iambatanayo na mchezo huo.
Kabla
hatujachukua hatua kubwa sana katika kujifunza haya, ninaomba tujenge uelewa wa
pamoja juu ya maswala kadhaa ambayo yana uhusiano wa moja kwa moja na maswala
mazima ya malengo.
·
Kusudi – ni sababu kuu ya kuwepo kwako. Hii
hujibu swali la “Kwanini ninaishi?” Kwanini kanisa hili lipo? (kanisa kama
taasisi kubwa na pia kama kanisa la mahala husika) mfano: Ninaishi ili kuudhihirisha utukufu wa Mungu kwenye kizazi
changu; Kanisa la “Fulani” lipo ili kuinua kizazi chenye kuleta athari kwenye
nyanja zote za kimaisha kwa msingi wa neno la Mungu.
·
Maono – ni taswira/picha kubwa uionayo juu
ya mwisho wa maisha yako, huduma, idara, kitengo na/au kanisa lako. Ni
mkusanyiko wa mwisho wa maisha yako. Hii hujibu swali la “ninakwenda/tunakwenda
wapi?” Ni muhimu ukumbuke sa utunze hii ya kwamba maono si ubunifu wa mtu bali
ni uvuvio wa kimungu ndani mwanadamu. Kama huna uhakika, basi usijaribu kubuni
maono! mfano: … Kumtukuza Mungu kwa kufanya
ugunduzi, uvumbuzi na utatuzi chanya wa mahitaji ya kizazi changu.
·
Dhamira – ni namna gani utafanya ili
kuyafikia maono hayo kivitendo. Hii hujibu swali la “Namna gani nitatekeleza/tutatekeleza?”
Mfano: … Kufungua taasisi ya utafiti
wa uwezo wa mwanadamu na uelimishaji wa vijana.
N.B
Unaweza kuwa na dhamira zaidi ya moja… Hakuna ukomo ilimradi tu dhamira
zinafanikisha ufikiaji wa maono yako.
Ni
wajibu wako kama kiongozi kufikiri na kuchambua namna mbalimbali za kuyaweka
maono hayo katika utendaji!
·
Malengo/Mipango – ni kuweka namna/njia za
kivitendo na zinazopimika ili kufanikisha dhamira yako/zako Mfano: … Kufanya usajili wa taasisi
yangu ifikapo March 28 ili kuanza utendaji rasmi.
·
Mkakati – ni mchanganuo wa hatua kwa hatua
na uratibu wa rasilimali ili kufanikisha malengo yako. Hii hujibu maswali mengi
“Nifanye nini, nifanye wapi, wakati gani, muhusika ni nani?...” Mfano: …
0 comments: