Mtangazaji kutoka kituo cha Praise power Radio Victor Aron mwenye umaarufu katika kipindi chake cha Faraja Time leo amepiga story na blog kueleza ujio wa video ya albamu yake 2 X 2=4.Albamu hii iliyo jichukulia umaarufu mkubwa kutokana na nyimbo kama Nitakusema kwa Baba,Nguo ya kuazima,na 2x2=4 kwa sasa ipo kwenye hatua za mwisho za utengenezaji wa video za nyimbo.
za albam hii.Victor alianza kazi ya utangazaji mwaka 2007 na mpaka leo ni mtangazaji wa Radio,kwa habari ya uimbaji alianza 1995 akiwa darasa la 7 katika kwaya ya vijana ujiji kigoma iliyojulikana kwa jina la UYGC.Mwaka 2005 akahamia dar ambako alipata bahati ya kushiriki shindano la Gospel Star Search ambapo alikumiongoni mwa 10 bora na hapo ndipo safari ya Victor kuwa solo artist ilipoanzia.Mpaka leo Victor anamiaka 8 ndani ya kazi ya uimbaji wa muziki wa injili akiwa na albam 3.Tizama picha za utengenezaji wa Video hii
On set..
I like this photo,big up mzee wa honyoraa.
Twende kazi.
0 comments: