Katika uhai wake,Marehemu Dr.Moses Kulola alikua na wajuku 47. Katika wajuku hao,Flora Mbasha ndiye alikua mjukuu kipenzi chake sana. Niliwahi kuongea na mume wa Flora Mbasha,Mr.Emmanuel Mbasha ambaye alinieleza jinsi ambavyo marehemu Dr Kulola alivyokua akimpenda sana Flora toka alipokua mdogo na mara zote katika kazi yake ya kuhubiri injili Dr. Moses Kulola alikuwa akisafiri na Flora.Ukiachana na hilo,Flora Mbasha alianza kuimba akiwa mdogo sana,marehem Askofu Kulola alishaiona huduma ya Flora tangu wakati huo, hivyo alikua akiiombea na kumtia moyo kwamba siku moja atafika mbali.
Ni wazi kabisa leo tunajionea jinsi ambavyo Flora Mbasha amekua maarufu na mwenye mafaniko mazuri katika kazi ya muziki wa injili.Upendo aliokuanao Flora Mbasha kwa Askofu Moses Kulola ni mkubwa sana. ambapo kabla ya kifo chake, Flora Mbasha alifanya nyimbo na marehemu Moses Kulola aliyoipa jina la Haleluya kwa mara ya kwanza itizame hapa mdau wangu.
0 comments: