Wednesday, August 14, 2013

MZIKI WA INJILI WAPATA KAMPUNI MPYA YA VIDEO.TAZAMA BEHIND THE SCENE YA UTENGENZEZAJI WA VIDEO YA LEVI NGOY.

By Jimmy  |  11:47 AM No comments

Kijana wa nguvu katika mziki wa Gospel Levi Ngoy akiwa kwenye pozi la shooting.
 
Katika kuleta mabadiliko kwenye muziki wa injili hasa katika utengenezaji wa video za Gospel EAGLE VIEW PRO imedhamiria kuleta mapinduzi mapya katika muonekano wa video za muziki wa injili Tanzania.Ni kilio changu kila siku kupata kampuni mpya zitakazoleta ubunifu na utofauti na video tulizo zizoea kuziona.Yapo makampuni mengi ya video za Gospel yaliyo jitaidi kututoa tulikotoka hadi sasa,lakini mpaka muda huu hakuna tofauti kubwa ya kusababisha muziki wetu kupenya Kenya,Uganda,Rwanda na hata ulaya.
Habari Maalum,Mbc hot media,Ajm Production,Brayance media na Ltv ni makampuni makubwa yenye majina hapa Tanzania yaliyosaidia kwa kiasi kikubwa kuufikisha mziki wa Gospel hapa ulipo,lakini katika hilo zimekua zikifanya kazi kama mazoea na kuto jali umuhimu wa kazi ya msani hasa katika kuandaa Script,location,pamoja na kutafuta directors wazuri watakao weza kusaidia kuongoza video katika utengenezaji ili mziki wetu uweze kupenya katika nchi za nje na kusaidia waimbaji wa Gospel kuweza kupata mialiko na hata kuingia kwenye tuzo za wenzetu.
 Debro Gabriel ni director mpya katika tasinia ya muziki wa injili aliye dhamiria kuleta mapinduzi ya video za Gospel katika kizazi hiki kipya.Nimepata bahati ya kutizama kazi zake naona tofautu kubwa ya video zake ambazo soon kupitia Chomoza ya Clouds tv utakwenda kuziona mdau wangu.
Hii ni behind the scene ya utengenezaji wa video ya muimbaji wa mziki wa injili Levi Ngoy anaye kuja na album yenye jina 24-7 God Lives.
 Director Debro Gabriel akiwa kikazi zaidi

Kazi ya shooting ikiendelea
 Mdogo mdogo wataelewa...

 On set Coco beach
 Twende kaziii.

Warembo wa nguvu mdau wangu.Hapana chezea.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP