Kituo hiki kiko Bunju mwisho
kinachoangaliwa na Dada Sifa.Dina aliweza kukijua baada ya kupigiwa simu na
mwanamuziki Stara Thomas.Stara
alimpigia simu na kumuunganisha na dada Sifa ili aweze kufika katika kitu hicho.
Ana watoto 20 wanao lala na
wengine 30 wanaokuja na kuondoka.Hao 30 ni wale ambao wanakaa kwa mama
au bibi,babu ila mazingira magumu hawaendi shule wala kupata mahitaji
muhimu.Wanakuja kushinda hapo kuna walimu wanafundishwa,wanakula na
kushinda na hao wengine jioni wanarudi makwao.
Hapo watoto wanapokaa ni kwa
mama yake na Sifa sio kituo rasmi ila Mungu akimjaalia atanunua kiwanja
na kujenge nyumba ambayo watoto wanaweza kukaa vyema.Mama yake Sifa ndio
anamsaidia kwa kiasi kikubwa kulea watoto wakati yeye akiwa kwenye
pilika pilika za huduma ya mziki wa injili
Msaada mkubwa Sifa anaouhitaji
kwa watoto wake ni chakula,mavazi,viatu,vifaa vya shule,sabuni za kufua
na kuoga,dawa za meno,mafuta ya kupikia na kujipaka.
Pia ikiwezekana apate ml 4 za
kununua kiwanja atakachoweza kujenga hapo baadae eneo litakalokidhi
mahitaji ya watoto kuishi na kucheza vizuri.
Picha wa hisani ya Dina Marios.
0 comments: