Natangaza rasmi Samuel Sasali na Milembe John Madaha ni wachumba kwa sasa.
Siku ya J/pili ya Tarehe 23/6/2013 blogger,mtangazaji wa Clouds TV, Samuel Sasali ametangaza uchumba katika kanisa la VCC huku akisindikizwa na marafiki zake wengi kutoka katika makanisa mbalimbali.Ukweli ulio wazi mbuyu huu ulikuwa mgumu kupita maelezo kila greda lililopata nafasi ya kuung'oa haikuwezekana.Lakini usukani wa merikebu Dr.Milembe ndiye aliyeuwangusha mbuyu huu na kuweka historia kwenye maisha yake.Blog hii inawatakia maisha marefu yenye muonekano mpya na wenye furaha na amani katika kuelekea kwenye maisha yenu ya ndoa.Hongera mbuyu ulianguka chaliiii Samuel Sasali kwa kuvunja ukimya.
Addo November mwanamuziki wa injili akifurahia mbuyu kuanguka puu!!Kimyaaa
Hii picha pendeza mbayaaaaa
Baada ya Mchungaji Huruma Nkone kutangaza uchumba wao kilipigwa kitu cha sebene.Usifanye mchezo palikuwa hapatoshiiiii!!
Familia ya Mzee Sasali
Tuliopotoka kanisani kuliandaliwa chakula cha jioni na familia ya Mzee Sasali.Katika chakula hicho cha jioni walijumuika marafiki mbalimbali kufurahi na familia hii ikiwemo na familia ya Milembe John Madaha.
Mr & Mrs Sasali wakikaribisha wageni.
Kitu cha sebene kutoka kwa Glorious Celebration ikabidi na mimi nijiunge
Hatari weka mbali na watoto likipigwa sebene ukakutana na vijana wanaopenda mwendo wache kama walivyo.
Mzee Sasali akipata chakula na wageni mbalimbali.
Natamini ujue alichokua anacheka Samuel Sasali?siri yangu!
Natamini ujue alichokua anacheka Samuel Sasali?siri yangu!
0 comments: