Jukwaa la Wakristo
Tanzania (TCF) limemesema Wakristo wasilazimishwe, kula nyama zilizochinjwa
kwa MisingiyaIbada ya Kiislamu kwakuwa Wananchi wa Tanzania ni wa Dini tofauti tofauti
na za makabila mbalimbali na hivyo wameitaka
Serikali kutamka wazi kuwa kila Raia ana uhuru wakufuata imani yake katika Swala
la Uchinjaji.
Hayo yamesemwa jana na Viongozi wa Jukwaa la Wakristo
Tanzania TCF, wakiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)
Askofu Peter Kitula, Rais wa Baraza la
Maaskofu Tanzania (TEC) Askofu Tercisius Ngalalekumtwa , pamoja na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Makanisa ya Kipentecoste Tanzania
(PCT) Askofu David Batenzia mbapo
walisoma Tamko hilo kwa kupokezana.
Uongozi huo umesema kuwa, Kwakuwa kuchinja wanyama na Ndege ni
Ibada kwa Waislamu, Kanisa linapaswa kutambua na kuheshimu jambo hilo na Kuongeza
kuwa linaaminika kwamba Sheria ya Nchi inaweka Bayana juu ya Usalama wa nyama hizo
kiafya lakini Serikali haielekezi kuwa ni Dini ipi inayopaswa kuchinja mifugo
hiyo.
Wakristo hao wameitaka Serikali iweke wazi utaratibu wa Kugawana Machinjio na
Mabucha kati ya Wakristo na Waislamu ili kila Mtanzania awe huru kujinunulia kitoweo mahali anapotaka sambamba
na kuitaka serikali kutimiza hayo Wakristo hawatakuwa wamevunja Sheria yoyote ya
Nchi wakiamua kujichinjia kitoweo chao wenyewe.
“Kwa upande Mwingine kwa kuwa tayari zipo bidhaa za Nchi hii
ambazo zina Nembo ya Halal na nyingine hazina Nembo hiyo huu ni uthibitisho kuwa,
vyakula hivyo vimegawanywa kwa kufuata Misingi ya Imani ya Kidini kwahiyo Kugawana
Mabucha na Machinjio sio jambo jipya kwasasa hapa Nchini”, amesema Askofu Peter Kitula.
Viongozi hao pia Wameitaka Serikali iimarishe Ulinzi na Mali
za wakristo wote Nchini Hasa waliopo Zanzibar maana hiyo ni haki yao kikatiba.
0 comments: