Makanisa nchini Kenya siku zote yamekuwa yakitoa sauti juu ya ishu
zinazoathiri waumini wake na jamii kwa ujumla . baadhi ya viongozi wa
kidini wameilaani mamlaka ya mawasiliano (CCK), kwa kushindwa kuchukua
hatua dhidi ya tangazo la condom linalorushwa kupitia televisheni ya
taifa kabla ya taarifa ya habari.
kutokana na viongozi wa kanisa, tangazo hilo la condom lililopewa jina
la “Weka Condom Mpangoni”, lililotegemewa kuelimisha jamii juu ya
umuhimu wa matumizi ya condom, inashawishi mmomonyoka wa maadili kuliko
kuelimisha.Bishop Julius Kalu wa kanisa la Anglican nchini Kenya,
daiosisi ya Mombasa, amesema ni wazi kabisa tangazo hilo linaongeza
ushawishi katika matendo ya ndoa kwa wanafunzi wa shule na vishawishi
kwa walio ndani ya ndoa kutoka nje ya ndoa zao.
katika tangazo hilo ambalo limekuwa likiruka katika televisheni hiyo kwa
muda sasa, kuna sehem inayomuonyesha mwanamke akimwambia mwenzake kuwa
hata kama mume wake anakua hayupo, haimaanishi anakosa kustarehe
kwasababu jamaa yake mwingine anapatikana wakati wowote na yuko tayari
kumpa raha, na mwanamke wa pili anamshawishi kutumia condom wakati wote
akiwa anafanya starehe zake na huyo mpango wa kando wake
Baadhi ya wakristo wamefikia kusema kuwa tangazo hilo la Weka Condom
Mpangoni liko kinyume na maneno ya Mungu na kuchochea uzinzi.
Tizama video ya tangazo hilo hapa chini
0 comments: