Japokuwa nimejitahidi sana kuisahau siku hii lakini moyo wangu umeshindwa kufanya hivyo. Kila ninapotulia, iwe sebuleni au chumbani kwangu, picha ya siku hiyo huwa inanijia kichwani mwangu. Tukio hilo limekuwa kubwa kwangu huku likiendelea kujirudia kama mkanda wa filamu.
Nilipenda kwenda shule kusoma, na hii ilikuwa njia mojawapo ya kuepuka kufanya kazi za nyumbani, hasa kuosha vyombo kitu nilichokuwa nikikichukia mno.
Japokuwa nilikuwa mtoto mdogo lakini mama alijitahidi sana kuniweka katika
mazingira ambayo mtoto wa kike anatakiwa kuwa.
Achukia kuosha vyombo
Kila siku alikuwa akinitaka nioshe vyombo, hii ilikuwa kazi pekee niliyokuwa nikiichukia mno. Kila nilipokuwa nikirudi nyumbani, mama alikuwa akinipa maziwa na kiporo cha jana, nikimaliza kula, alikuwa akiniambia nioshe vyombo nilivyovitumia.

Nilikereka mno lakini sikuwa na jinsi, nilibaki
nikilalamikalalamika lakini mwisho wa siku niliosha vyombo mbele yake huku
akionekana kuwa na furaha.