Ongoza kimkakati
Weka malengo kwa vigezo hivi:
Malengo
mazuri huwa na sifa ya “SMART”, neno la kiingereza linalomaanisha nadhifu,
-enye uelewa mzuri. Kwahiyo malengo yako yanapaswa kuwa nadhifu, sasa neno smart
linabeba maana kubwa sana kwa kila herufi yake:
S -(Specific), kwanza lazima
lengo liwe ni maalum au hususani juu ya jambo, mtu au hali fulani. Kwa
mfano mtu anaposema, “Mimi ninataka kupambana na umaskini.”. Ni sawa hilo ni
lengo lakini si hususani, yaani halina mwelekeo… Je, mtu huyo anataka kupambana
na umaskini wa aina gani (umaskini wa kifikra, kifedha…), Je, anapambana nao
katika ngazi ipi? (mtu binafsi, kijiji, familia, nchi…) lazima uainishe
. Na
ndivyo ilivyo katika huduma, unaweza kusema nina wito wa kuhubiri injili, ni
sawa lakini ni katika ngazi gani? Ni wazi kwamba kuizungukia dunia yote ni
jambo ambalo si rahisi (nchi zote, mikoa yote, majimbo yote, wilaya zote, vijiji
vyote na kaya zote za dunia.) Si jambo rahisi, ukijaribu utaumia tu na matunda
hayatakaa.
Mfano: Lengo langu ni kuihubiri injili nchini
Tanzania.
Kumbuka kuwa Tanzania ni nchi kubwa, ina mikoa zaidi ya ishirini na
wilaya zake na tarafa, kata, mitaa/vijiji na kaya (familia) kwahiyo unatakiwa
kuwa specific zaidi. Kwahiyo waweza kusema, kuhubiri injili nchini Tanzania
katika ngazi ya wilaya.
M -(Measurable), Pili lengo
lolote linatakiwa kupimika, Je unaweza kuuona ufanisi, matokeo au
matunda ya lengo hilo? Kwa mfano lengo la kuihubiri injili nchini Tanzania
katika ngazi ya wilaya…Baada ya muda je unaweza kupima matokeo ya lengo hilo. Sasa
kuna njia mbalimbali za kuyapima malengo yetu, baadhi ya njia ni kuangalia
mabadiliko katika maisha ya watu, je, kuna mabadiliko yoyote,njia nyingine ni
kuangalia je, idadi iliyokusudiwa imefikiwa? Tukiendelea kuutumia mfano wetu wa
kuihubiri injili nchini Tanzania katika ngazi ya wilaya ili tuufanye kuwa
SMART; Ili kuweza kupima lengo hilo waweza kusema:
Kuihubiri injili kwa watu 1000 nchini Tanzania katika
wilaya 4 (unapaswa kuzitaja wilaya ulizokusudia kuzifikia) kuanzia Januari
mpaka Juni.
Je, unaweza kuyapima matokeo ya lengo hilo? Kwasababu unaijua idadi ya
watu unaotaka kuwafikia ni watu 1000 na tayari unajua wapi pa kuwapata (wilaya
4, Tanzania) kwa maana hiyo basi ni watu 250 kwa kila wilaya. Kwahiyo hatimaye unaweza
kuangalia Je, hizo wilaya 4 zilifikiwa na injili na Je, watu 1000 walifikiwa
pia? Hivyo ndiyo kupima malengo!
A (Attainable), Jambo jingine
la tatu na la msingi kufahamu ni kwamba lengo lolote linapaswa kufikika. Hapa
unapaswa kuangalia kwamba Je ,ninao uwezo wa kukamilisha lengo hilo kwa kiwango
hicho, Je,ninao watu wa kushirikiana nao kufika huko,Je ninahitaji maandalizi
ya kimaombi, kifedha, kifursa n.k kiasi gani? Kuna malengo mengine ukiyatazama
unatambua tu kwamba mtu huyu anaota ndoto za mchana, kwa kutumia mfano
wetu wa injili nchini Tanzania, unakuta mtu anasema: Lengo langu ni
kuihubiri injili nchi yote ya Tanzania kwa mwaka. Hilo ni lengo zuri na
lina nia njema lakini Je, unaweza kuifikia nchi yote ya Tazania kwa mwaka?
maana yake mikoa zaidi ya 20, yaani wastani wa wilaya 5 kila mkoa, sawasawa na
wilaya 100. Mwaka una siku 365, ambapo ni sawasawa na wastani wa siku 3 kila
wilaya. Unaweza? Vipi kuhusu muda wa
kujiandaa? gharama? familia? mapumziko? Usafiri,si unajua wakati mwingine
inachukua siku nzima kusafiri toka mkoa mmoja kwenda mwingine? Mikutano hiyo au
huduma hiyo utaiandaaje? Je, lengo hilo linafikia?, basi hata kama
likifikika halitakuwa na ufanisi.
0 comments: