Ongoza kimkakati
Mkakati
wa usajili wa taasisi:
Lengo la kuainisha, walau kwa ufupi
tu, tofauti ya mambo hayo ni ili uwe na uhakika na kitu gani unakiendea na
unapaswa kufanya. Ni muhimu sana ufahamu ya kwamba kusudi ndilo huwa sababu ya
maono; maono huzaa dhamira (utume) na dhamira ndiyo huleta malengo ambayo huzaa
mikakati tayari kwa utekelezaji. Ili kurahisisha uelewa juu ya mambo haya,
tazama na kujifunza kwenye Taswira ifuatayo:
Kwahiyo, somo hili litaanza kwenye
mzunguko wa malengo na ni wajibu wako kujua kusudi lako, maono na dhamira yako.
Ninaanza kwa kuamini kwamba (based on the
assumption that), wewe, ndugu msomaji wangu, umekwishawekeza muda wako
kulitafuta kusudi la Mungu juu ya maisha yako, unayajua maono yako na
umeyafikisha kwenye hatua ya dhamira (utume).
0 comments: