Ongoza kimkakati.
Lengo kuu la somo:
Kumuwezesha
kiongozi binafsi na timu ya viongozi wa kanisa la mahala husika (local church)
kwa ujumla kuwa na ufanisi na mwelekeo katika uongozi na usimamizi wa siku kwa
siku wa kanisa na idara zake.
Malengo mahususi ya somo:
i.
Kuelekeza kwa upana juu ya usuli (essence)
wa uongozi na usimamizi wenye kuelekea
kusudi kimkakati.
ii.
Kujifunza kutoka kwenye maisha ya viongozi
waliotutangulia juu ya uongozi na usimamizi wa kimkakati na kumahalisha
(contextualize) mafunzo hayo.
iii.
Kujenga stadi na mbinu za kuweka,
kutekeleza na kutathmini malengo kwa kiongozi binafsi na timu ya uongozi.
iv.
Kuliandaa kanisa la mahala husika kwaajili
ya kuwa chachu ya mabadiliko kwenye jamii na taifa kwa ujumla.
Matokeo yanyotarajiwa:
Baada ya kujifunza moduli hii, inatarajiwa:
·
Mithali 29:18,
“Pasipo maono, watu huacha kujizuia…”
Habakuki 2-3,
“BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao,
ili kila aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa,
inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia,
ingoje; Kwakuwa haina budi kuja, haitakawia.”
Ni
Muhimu sana ukatunza kumbukumbu ya malengo hayo ili uyapime na ujipime
kulingana nayo wakati wote wa mfululizo huu.
Hebu
jiulize pamoja na mimi juu ya mambo haya:
Kisa mkasa (Scenario) #1. Msafiri asiyejua aendako:
Nimewahi kuzungumza mahali
pengi na kwenye kitabu changu cha “Wokovu ni uhakika wa maisha ya Sasa na ya
Baadaye.” Juu ya mfano huu… Hebu jaribu
kufikiri ukiwa katika stendi kubwa ya mabasi yaendayo katika mikoa mbalimbali
(mfano stendi ya Ubungo- Dar Es Salaam, Nyegezi/Buzuruga- Mwanza, Msamvu-
Morogoro n.k) Anatokea mtu mmoja ambaye kwa mwonekano wake ni msafiri… amebeba
mabegi na mizigo kadhaa, mkononi ameshikilia chupa ya maji ya kunywa… akakujia
kisha akakuuliza, “Ndugu, naomba unionyeshe basi kwani ninataka kusafiri.” Je,
utamuonyesha basi gani? Au utamuonyesha basi la kwenda wapi?...
Kwa kadiri nijuavyo
mimi ni kwamba mtu mwenye akili timamu na nia njema, kama wewe ndugu msomaji
wangu, utahitaji kupata maelezo kamilifu… utataka kujua kule anakoelekea yaani
mwisho wa safari yake ili umwonyeshe basi linaloelekea mwisho
0 comments: