Sunday, July 20, 2014

Kanisa la Moraviani Mbeya wamaliza Mgogoro kwa masharti.

By Jimmy  |  3:49 PM No comments

Picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao

Mgogoro ulio likumba kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi (Mbeya) baina ya waumini walioungana na baadhi ya wachungaji dhidi ya Askofu wa jimbo hilo Alikisa Cheyo umemaliza baada ya kufishana mbele ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.



Hatua hiyo ilifikiwa Julai 16 mwaka huu baada ya mgogoro huo kudumu kwa zaidi
ya mwaka mmoja baina ya pande hizo mbili zilizotofautiana ndani ya kanisa hilo, kufikishwa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama, chini ya Mwenyekiti wake, Mkuu wa Wilaya, Dk. Norman Sigalla.



Mgororo huo umefikia katika hatua hiyo ikiwa ni siku tano tangu  baadhi ya wachungaji na waumini wa kanisa hilo  ambao walikuwa na makufuri, na Minyororo kuvamia na kisha kuteka na kufunga,lango kuu pamoja na milango

 yote ya ofisi wakishinikiza kujiuzuru kwa Askofu huyo



Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya kikaoo hicho kilicho fanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya na kudumu kwa zaidi ya saa tatu,pande zote mbili zinazo tofautiana zilikiri wazi  kwamba zilikiuka  taratibu za kanisa na kuvunja katiba.



Akizungumza na Mbeya yetu moja wawajumbe walioshiriki kikao hicho na kuomba jina lake liifadhiwa alisema kuwa kikao hicho kilikuwa na zaidi ya 30 na  muafaka ulifikiwa baada ya Askofu  Cheyo kuonesha hekima na busara kubwa ambapo alionyesha dhairi alikuwa na dhamira ya kweli ya kuliokoa kanisa hilo katika migogoro na kwamba hekima hiyo ingeonyeshwa tangu awali wasingelifika hapo walipofikia.



Akifafanua zaidi, mpaka Askofu huyo kufikia hatua kutoa maneno ya hekima ni baada ya Mkuu wa Wilaya, Dk. Sigalla kuonesha jinsi serikali ilivyochukizwa na mgogoro huo, ambao ulionekana kuvuka mipaka na kuashiria uvunjifu wa amani katika Wilaya yake na Mkoa kwa ujumla.



“Ni seme wazi  maneno ya Mkuu wa Wilaya kwamba serikali haiwezi kulinda fikra za waumini waliochukia, ingawa itaweza kupeleka askari, lakini haiwezi kulinda mipango ya kuchoma makanisa yalimgusa sana  Askofu Cheyo wetu na mungu akamuongoza na kuonesha busara na hekima juu ya suala hilo” alisema Mjumbe huyo



Taarifa zinaeleza kuwa  Askofu Cheyo, ambaye ni baba wa kiroho ndani ya kanisa hilo, alipopewa nafasi ya kueleza  hali ya mgogoro huo na nini kifanyike, alisema kimsingi, Mwenyekiti aliyesimamishwa Nosigwe Buya alifanya makosa ya kiutendaji pekee.



Hivyo, ili aweze kusamehewa na kurudishwa katika nafasi yake , anapaswa kuomba radhi kwa makosa yake ya kiutendaji na ndipo Halmashauri Kuu iweze kumfikiria na hatimaye kumrudisha kwenye nafasi yake.



Taarifa zaidi toka ndani ya kikao hicho, zinadai kuwa Baada ya maneno hayo ya Askofu, ndipo Mwenyekiti aliyesimamishwa Buya alisema kimsingi hana tatizo, lakini haamini kama kauli hiyo ya askofu ina ukweli.



“Sina uhakika na Askofu kwa kuwa amekuwa na tabia ya kubadilika badilika na kushindwa kusimama kwenye kauli zake mara nyingi, hivyo kama atakihakikishia ukweli kikao hiki, basi mimi sita kuwa na mengi zaidi ila isipokuwa lazima nimiweke masharti” chanzo hicho kilimnukuu Mwenyekiti Buya.



Mara baada ya kauli hiyo  Buya alidaiwa kutoa  masharti mawili, ambayo ni kutaka Makamu Mwenyekiti Zacharia Sichone,ambaye ndiye mtendaji Mkuu wa shughuli zote za kanisa na Halmashauri kuu  kusambaza taarifa ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ubadhirifu fedha zaidi ya shiloindi milioni 200/ itolewa na kusambazwa katika shirika zote 213 na idara zote za kanisa hilo.



Wakati sharti la pili lililo tolewa na Mwenyekiti huyo aliye simamishwa ni  kama taarifa hiyo ya ubadhirifu itaoneka si za kweli basi aombwe radhi ili kosa la kiutendaji lidhihirike, baada ya  vinara hao kutoa masharti hayo, yalionekana kuungwa  mkono na wajumbe wote, na huyo ukawa ndo mwisho na  muafaka wa mgogoro huo.



Mjumbe huyo alibainisha kuwa mbali na Busara za Askofu na Mkuu wa Wilaya,alisema shukurani za pekee ni Mchungaji Hakimu  Mwandenuka kutoka Usharika wa Tunduma ambaye ni mmoja wa wajumbe pale Mungu aliupo Muongoza kutumia vifungu vya kutoka biblia takatifu  katika kitabu cha Waebrania sura ya 12 , aya ya 14 hadi 15,  maneno yaliyo wagusa karibia wajumbe wote.



 “Una jua maneno aliyo yasoma Mchungaji  Mwandemula yaliwagusa sana wajumbe nayo yanasomeka ‘Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo ndio utakatifu ambao hapana mtu atakayemuona bwana, asipokuwa nao, kwani shina la uchungu lisije chipuka na kuwasumbua na watu wengi watatiwa unajisi kwa hilo ”.alisema Mjumbe huyo



Kanisa hilo liliingia katika mgogoro  huku wachungaji 20 na baadhi ya waumini, wakiwemo wazee wa mabaraza ya kanisa hilo, wakipinga uamuzi uliofanywa na Halmashauri kuu yaJimbo hilo huku Askofu Cheyo akitajwa kuwa kinara katika uamuzi wa kumuondoa katika nafasi yake aliyekuwa Mwenyekiti Buya hatua iliyo pelekea baadhi ya sharika  kususa kupeleka sadaka ofisi kuu ya jimbo.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP