SAFU
YA FRED MSUNGU: BADILI CHANZO CHA TAARIFA
JINSI
ULIVYO LEO NI MATOKEO YA ULICHOKISIKIA NA KUKIAMINI
UTANGULIZI
Katika maisha ya
kila siku, kila mmoja kwa upande wake kuna mambo ambayo anayatarajia sana kama matokeo halisi ya kitu fulani aliwahi
kupanga au kuwaza katika maisha yake.Japo kua matarajio hayo hua ni siri ya mtu
binafsi lakini nina uhakika kwa asilimia nyingi sana kwamba kila mmoja wetu
anamatarajio mazuri katika maisha yake.Pamoja na kua kila mmoja wetu anategemea
matokeo mazuri (chanya) lakini kuna kitu cha kwanza kufanya ambacho hicho ndio huleta matokeo
unayoyahitaji,Inawezekana ukawa na matarajio mazuri sana lakini kua na matarajio
(imani juu ya kitu fulani)na mambo makuu na mazuri hiyo haimaanishi tayari umepata uhakika au tiketi
ya kuyafikia matarajio hayona kuyafanya kua kitu harusi.Wapo watu wengi
waliokua na ndoto kubwa (matarajio)lakini hawakuweza kufikia, Na hii ni kwasababu
tu!Hawakutengeza mwanzo wao kuakisi matokeo ya kesho yao.Kua na wazo au
tarajio zuri peke yake si ufunguo wa
mafanikio kuyafikia malengo,
kuna mambo ambayo kupitia kwayo hayo ndio huzaa
matokeo chanya moja kati ya jambo la msingi sana kati ya hayo ni CHANZO CHA
TAARIFA:
TAARIFA NI NINI?
Taarifa ni
ujumbe wowote unaokujia kwa njia tofauti
tofauti...inaweza kua kwa :-
·
Kuambiwa /kusimuliwa
·
Kusikiliza
·
Kusoma
·
Kuona
Viko vitu vingi
ambavyo vinaweza kua ni sababu ya wewe kupata taarifa, lakini hizo ni njia au
vyanzo vichache ambavyo mara nyingi vimetumika sana kutoa taarifa au elimu ya
kitu fulani. Kitu cha muhimu Sana hapa kujua ni kwamba taarifa ni taarifa Haijalishi
ni taarifa nzuri au mbaya!Ukishaipokea kwa kupitia moja kati ya hizo njia nilizoziorodhesha
basi tayari hiyo ni taarifa.Na kwa namna moja au nyingine tegemea kuathiriwa
na ile taarifa ulioipokea.
LENGO LA TAARIFA NI NINI?
Lengo kuu la
taarifa hua ni kujuza, kuaminisha, Kuonya, kuelimisha na wakati mwingine
kupotosha .Hayo yote ni malengo ya taarifa ambayo mara nyingi yanatokea
kutokana na mtoaji taarifa anamlengo
gani au mpokeaji wa hiyo taarifa amechagua kusikia nini au kumsikiliza nani.
Kitaalamu,
kiuumbaji (kisayansi) moja kati ya kazi kubwa ya ubongo ni kupokea taarifa mbali
mbali (kufikiri) Na huwezi kufikiri bilakua na kitu cha kukifikiria, Sasa hicho
kitu cha kufikiri ndio hiyo taarifa ambayo inatokana na vile vyanzo
nilivyoviorodhesha awali.
MUHIMU: Ninachotaka kukujuza
hapa ni kwamba uwe unapenda au haupendi swala la kupokea taarifa kwako si la
hiyari kwako, Ni lazima kuna taarifa ubongo wako utapokea tu! na baada ya
ubongo kupokea taarifa ni lazima ubongo ufanye kazi ya kufikiri, na fikra
hutokea kutokana na aina ya taarifa uliyoisikia na matokeo yeyote unayoyaona
yametokea nje chanzo chake hua ni taarifa.Swala kupokea taarifa si hiyari
lakini ni aina ipi ya taarifa umechagua
kupokea hilo ni uchaguzi wako.
Kwa maneno
machace tu hapa naweza kukujuza kwamba ......CHANZO SAHIHI CHA TAARIFA HULETA
FIKRA SAHIHI....NA FIKRA SAHIHI HULETA MATOKEO SAHIHI.vivyo hivyo CHANZO KIBOVU
(POTOFU) CHA TAARIFA HULETA FIKRA MBOVU NA FIKRA MBOVU HULETA MATOKEO MABOVU
JINSI TAARIFA INAVYOATHIRI MAAMUZI YAKO
Maamuzi ni
chanzo kikubwa cha matokeo, Hakuna jambo lolote lilitokea bila mtu kufanya
maamuzi ya kuliweka jambo katika vitendo, Wazo pekee halitoshi kuleta matokeo
yanayoonekana ...maamuzi ni hatua inayosababisha tendo na tendo huleta matokeo
lakini haya maamuzi yanaathiriwa sana na chanzo cha taarifa. (Warumi 10:17 Basi imani chanzo chake ni
kusikia na kusikia huja kwa neon la kristo) Ukisoma Kwa umakini hapo
utatambua kitu kikubwa sana. Ukifikia hatua ya kuamua kitu basi lazima kuna
taarifa iliyokushawishi kukupelekea wewe kuamua.Imani ni matokeo tayari ambayo
chanzo chake kimekuja kwa njia ya kusikia lakini chanzo cha taarifa hapa ni
nini? Au kusikia kutoka kwenye chanzo gani cha taarifa? Hili ni swali kubwa
ambalo unatakiwa kujiuliza.Kwa mujibu wa andiko hapo juu utaona kwamba
kulisikia neno la kristo hicho ndo
chanzo kikuu cha taaarifa.Sasa kama matokeo ya kuamini au imani hua ni kusikia
jiadhari sana na nini unachagua kusikia kwani hicho ndicho huleta matokeo ya
jambo.Unaweza ukawa unajiuliza sana kwanini mara nyingi katika safu hii nimetumia
neno ‘UNACHAGUA KUSIKIA’?Kitu kikubwa ninaamini katika maisha hali yeyote
ulionayo ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe,kama ni umasikini au
utajiri,kufaulu au kufeli,kushinda ama kushindwa hivi vitu vyote ni uchaguzi wa
mtu binafsi.Hii inaweza ikakupa shida kidogo lakini nitakueleza kwanini imani
yangu inanituma hivyo.
Itaendelea wiki ijayo.............................................
Itaendelea wiki ijayo.............................................
Asante sana.
ReplyDeletenimebarikiwa sana
ReplyDelete