Leo 10/9 mchana kwaya ya uinjilisti Kijitonyama imefanya press conference ya tamasha la uzinduzi wa CD na DVD yao ambayo inaenda na kwa jina la "Namtangaza kristo" ambayo itafanyika tarehe 13/10 kwenye kanisa lao lililopo Kijitonyama.
Akiongea kwenye press conference hiyo mwenyekiti wa kwaya hii maarufu kama MC Fomafoma alisema
"Siku hiyo kutakuwa na live band pamoja na kwaya nyingine kuja kuwapa support siku hiyo.DVD pamoja na CD zitauzwa siku hiyo pamoja na fulana za Namtangaza kristo pamoja na key holder za Kijitonyama. Msikose watu wote siku hiyo na kiingilio kitakuwa ni bure kabisa".
0 comments: