Siku Ya Jana Katika
Garden Ya Tamal Hotel Friends On Friday Kama Kawaida ilichukua mkondo
wake, ambapo groups mbalimbali za Muziki wa Injili zilionesha Ustadi
Mkubwa katika Live Performance.
Kikosi Kipya Cha
Glorious Celebration kilionesha Makali yake kwa Vocal na "wese" juu yao
na kuwashangaza wengi waliohudhuria katika Usiku wa Jana, Muonekano wao
wa Sare uliwafanya kuonekana maridhawa kabisa.
Paul Clement
mwanamuzi kutoka kundi la Glorious Worship Team kama ilivyo ada na
kawaida alikwenda sawa kabisa nakuonesha ukongwe wake wa Muziki wa
Injili katika muda mfupi aliokaa katika tasnia hii, nyimbo zake za
kuabudu alioshusha uwepo mahali hapo usiku wa jana.
Felis Mubibya
Mwanamuziki wa Kundi la Sowers ambaye anafanya muziki wa Injili nchini
Marekani nae alikuwepo kwa ajili kunogesha shughuli nzima ya Friends On
Friday. Akiongea na blog hii Felis alisema "muziki wa injili wa Tanzania
unakuwa sana, tofauti na Marekani na Ulaya ambapo watu hucheza pia kwa
kujificha ficha, lakini upigaji na arrangements za muziki wa live huleta
radha kamili.
Wadau wakubwa wa Friends On Friday Miriam Lukindo wa Mauki na Steven Wambura walinogesha zaidi katika Event Ya Jana Usiku.
Papaa akienda Sawa na 12 Disciples ndani ya Tamal
Kulia ni Furaha Masinga, Kati ni Edna Luvanda Kushoto ni Milembe wa Blogger Sasali.
Kitu Cha Ajabu
zaidi zaidi Ya watu 10 usiku wa Jana wamejitolea ku-support Friends On
Friday Kila Mwezi Kuhakikisha Inafanyika. Wamejitolea Kutoa Fedha zao,
na wakati Huo Huo Tv Sibuka Kupitia Kipindi Chake Cha Gospel Hits na
Clouds Tv Kupitia Kipindi Cha Chomoza wamejitolea Kuwa Wadhamini
Wamojawapo wa Friends On Friday Kwa Mwaka 2013.
Tofauti
na ilivyotarajiwa na watu kuona makundi hayo kama maadui, waliweza
kushirikiana vyema viwanjani hapo ikiwa pamoja na kucheza pamoja
walipoguswa, wapigaji wao kushirikiana kuwapigia waimbaji wengine na
kukaa pamoja jambo ambalo watu wengi wamemtukuza Mungu kwa ajili ya
makundi hayo.
Mdau Mkubwa nambari wa FoF Shemeji Jacque Mndeme na mumewe aliye jificha na Camer.
Mzee wa Saxerphone
0 comments: