Tuesday, September 16, 2014

KIANGO MEDIA NA KINGDOM MEDIA ZA SAINI MIKATABA YA KUWATANGAZA WANAMUZIKI WA INJILI KIMATAIFA.

By Jimmy  |  9:39 PM No comments

Mkurugenzi wa Kiango Media (kulia) na Mkurugenzi wa Kingdom Media Wakibadilishana Mikataba iliyotiwa saini

Kampuni Ya Kingdom Media yenye Makao Makuu yake Nchini Marekani siku ya leo Imewekeana Mkataba na Kampuni ya Kiango Media yenye maskani yake Jijini Dar-es-Salaam.

Siku Ya Leo Katika Hotel moja jijini Dar-es-Salaam, Makampuni haya mawili yameamua kutiliana saini kwa ajili ya Kufanya kazi ya Muziki wa Injili kwa Manufaa ya Wanamuziki wa Injili hapa
Tanzania.
 Akizungumza na Waandishi wa Habari siku ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa Kingdom Media, Bw. Alex amesema kuwa "Mkataba huu utawanufaisha kwa kuwatangaza Wanamuziki wa Injili wa Tanzania katika nchi za America pamoja Ulaya ambako Kingdom Media imeweka makazi yake"

Naye Mkurugenzi wa Kiango Media Sam Sasali Ze Blogger akiongea mbele za Waandishi wa habari alisema "Huu ni Mkataba wa pili ndani ya wiki hii kwa Kampuni yetu ya Kiango, kuweza kutiliana saini na makampuni ya kimataifa katika kutangaza kazi za |Wanamuziki wa Injili"

Akifafanua baadhi ya makubaliano yaliyoingiwa siku ya leo Ze Blogger alisema "Mara nyingi sana tumekuwa tukiwapokea wanamuziki kutoka Africa Ya Kusini, Congo, Kenya na kwingineko, Sasa ni zamu yao kutupokea Tanzania, Kupitia Mikataba tunayoingia na Makampuni ya Kimataifa nia hasa ni kupeleka kazi ya Muziki wa Injili nje ya Mipaka ya Tanzania"
 Mkurugenzi wa Kiango Media (kulia) na Mkurugenzi wa Kingdom Media Wakibadilishana Mikataba iliyotiwa saini
 Mkurugenzi wa Kingdom Media akijiridhisha kwa kusoma Mkataba
  Mkurugenzi wa Vipindi na Habari wa Kiango Media Kulia James Temu, Mkurugenzi wa Kiango Media Tanzania, Mkurugenzi wa Kingdom Media ya Marekani na Mwakilishi wa Kingdom Media Tanzania wakipiga picha mara baada ya kuzungumza na Wana Habari

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Kiango Media alieleza Waandishi wa habari kuwa Utaratibu wa kufanya kazi na wanamuziki wa Injili hapa Tanzania utaandaliwa na kuwasilishwa kwa uongozi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania ili kuweza kupata mawazo pia ya wanamuziki namna bora ya kuendesha mikataba yake pamoja na wanamuziki.
Huu ni Mkataba wa pili ndani ya wiki moja ambapo mapema wiki hii Kiango Media Iliingia Mkataba na Mikito.Com kwa ajili ya kuuza nyimbo za wanamuziki wa Injili kupitia Mitandao Ya Kijamii.
Kiango Media Company inatazamia kuzindua Radio, Television pamoja na Magazine ya "Gospel Today" kati ya mwezi October, 2014 na January, 2015.
Mwakilishi wa Kingdom Media akianguka Saini huku akishuhudiwa na Wawakilishi wa pande zote mbili.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP