Monday, September 15, 2014

BEI YA KIINGILIO KWENYE UZINDUZI WA JOHN LISU HADHARANI.

By Jimmy  |  9:59 AM No comments


Waandaaji wa uzinduzi wa albamu ya “Uko Hapa” ya mwimbaji nguli wa muziki wa Injili Tanzania, John Lisu unaotarajia kufanyika Oktoba 5, mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, kampuni ya
Msama Promotions wametangaza viingilio rasmi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama viingilio hivyo ni shilingi 5000 kwa viti vya kawaida na watoto na shilingi 10,000 kwa viti maalum.
Msama ametoa wito kwa waamini mbalimbali nchini kujitokeza katika uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake katika tasnia ya muziki wa Injili nchini.
Msama amesema hivi sasa waimbaji watakaoshiriki katika uzinduzi huo wako kwenye mazoezi makali kwa ajili ya kujiandaa na uzinduzi huo.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP